Na Mary John, Simanjiro

Diwani wa Kata ya Endiamtu Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara Lucas Zacharia Chimba ameyataja magonjwa 10 yaliyoongoza katika kipindi cha mwezi January hadi Machi Kwa Mwaka huu wa 2023.

Hayo amebainisha jana kwenye kikao Cha baraza la madiwani, wakati akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Maendeleo ya kata ya Endiamtu,mbele ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Jacob Kimeso, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Samwel Warioba Kunzar, chenye lengo la kujadili taarifa zote za kata 18 Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Chimba amesema katika kipindi cha mwezi wa January hadi Machi Mwaka huu jumlamya magonjwa 10 yameonekana kuongoza kwa wagonjwa walifika kupata huduma katika Kituo cha Afya Cha Endiamtu Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Akiyataja magonjwa hayo Chimba amesema kuwa ni pamoja na ugonjwa wa tumbo, kifua, upungufu wa damu, kuhara, shinikizo la damu, kisukari, mafindofindo, ukimwi, mimba zinazoharibika pamoja na ajali za Barabara.

Aidha amesema Kituo Cha Afya Cha Kata ya Endiamtu licha ya kuwa kinatia huduma Wilaya ya Simanjiro lakini pia kinatia huduma katika Wilaya 2 za Arumeru na Hai na kupelekea Kiria hiko kutoa huduma jumlamya Wilaya 3.

Amesema Kwa kipindi cha mwezi January hadi Machi, 2023 Kituo hiko kimepokea jumla ya wagonjwa wapatao 23,184 walioweza kupata huduma ya matibabu, hiyo ikiwa ni sawa na wastani wa wagonjwa7,728 wanaotibiwa kwa kila mwezi.

" Wagonjwa hao ni sawa na wastani wa wagonjwa 276 wanaohudumiwa kwa siku, huku wagonjwa 623 hulazwa katika Kituo hiki Cha Afya Endiamtu" amesema Diwani Chimba.

" Kuna changamoto nyingi zinazoikabili Kituo chetu Cha Afya Cha Endiamtu, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa wood ya wagonjwa wa TB, ukosefu wa Mashine ya usingizi wakati wa ufanywaji wa upasuaji mkubwa, hivyo tunaiomba Halmashauri iweze kuziangalia hizi changamoto nakuona namna ya kuzitatua haraka iwezekanavyo ili kuwezesha Kituo hiko kuweza kutoa huduma husika kikamilifu" ameongeza Diwani Chimba.

Hata hivyo ameiomba Serikali kununua Mashine muhimu zinazohitajika katika utoaji wa huduma kwenye kituo hicho, ili kukiwezesha kituo hiko kutokana na huduma zake kwa Ufasaha.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...