Watoto watatu kutoka Shule ya Msingi Itubukilo B, Kijiji cha Pugu, Kata ya Itubukilo Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu wamefariki dunia Aprili 25 baada ya mkokoteni waliokuwa wakisafiria baada kuchota mchanga MTONI kusombwa maji ukiwa unavutwa na ng’ombe sita. Waliofariki ni Maleki Legi (16), Isaka Njile (14) na Wille Njile ambao ni watoto wa familia moja huku watoto wawili wakinusurika.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga @official_simalengatz akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya hiyo amefika katika eneo hilo na kujumuika na wananchi ambapo pamoja na kuwapa pole wafiwa amewaasa wazazi juu ya umuhimu wa kuzingatia malezi ya watoto hasa kipindi hiki cha mvua kubwa
“Ndugu zangu Wanakijiji cha Pugu kwa niaba ya Serikali nimesikitishwa na kusononeshwa na tukio hili la kusikitisha Na kusononesha limekatisha maisha ya watoto wetu hawa ambao walitakiwa kuwa nyumbani wakati huu wa msimu wa mvua. Poleni sana Wazazi, ndugu na wanakijiji wote. Nawasihi sana tuwe makini katika malezi ya watoto hususani katika kipindi hiki cha mvua. Ni jambo la kusikitisha ni kusikia kuwa watoto hawa wadogo walipewa jukumu la kwenda mtoni kuchota mchanga tena wakiwa na mkokote uliokuwa unavutwa na ng’ombe 6 tofauti na umri wao”. Alisihi SIMALENGA
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Na uokoaji Mkoa wa Simiyu Inspector Faustine Mtitu amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari pindi wavukapo mito na madimbwi kwani kumekuwa na maji mengi ambayo yanaweza kuleta maafa.
Wananchi wa kijiji cha Pugu wameiomba serikali kujenga kivuka cha daraja ili kuwa suluhisho kwa wananchi wa maeneo hayo kwani mto huo umekuwa ni hatari kwa maisha ya watoto wao kutokana na wanafunzi kutumia mto huo katika kuvuka kwenda shuleni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...