*Yawataka kusajili vilainishi vya magari/ mitambo kabla ya Mei 15, 2023.

Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo uuzaji vilainishi visivyokidhi ubora katika baadhi ya maeneo nchini kinyume na sheria.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dk.James Andilile imeeleza kuwa mfanyabiashara atakayekutwa na vilainishi visivyokidhi viwango atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutozwa faini isiyopungua sh.Milioni kwa 10 kwa anayezalisha, milioni Saba kwa muuzaji wa jumla huku msambazaji akipaswa kulipa sh.milioni Sita na muuzaji wa rejareja sh.milioni Tano.

Aidha taarifa hiyo imesisitiza kuwa, adhabu hizo zinaweza kuambatana na vifungo mbalimbali kwa mujibu wa sheria.

EWURA imetoa onyo kwa wazalishaji, waagizaji na wauzaji wa jumla kuacha mara moja kuuza bidhaa za vilainishi vya magari/mitambo visivyokidhi ubora pamoja na kuwataka wafanyabiashara kusajili vilainishi EWURA kabla Mei 15 , 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...