Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Profesa Christine Noe akionesha kitabu wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 2, 2023 jijini Dar es Salaam kuelekea uzinduzi wa Kitabu kitakacho zinduliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa (MB) Aprili 4, 2023 chuoni hapo. Katikati ni Mhadhiri kutoka Idara ya Geografia, Faraja Namkesa na Mhadhiri wa Idara ya Sosiolojia na Antrolojia, Ndaki ya Sayansi za Jamii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Rechard Sambaiga.
Mhadhiri wa Idara ya Geografia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Pilly Siluano akifafanua jambo juu ya ushiriki wa wanawake katika miradi mbalimbali katika maeneo yanayotekelezwa miradi kwa waandishi wa habari leo Aprili 2, 2023 jijini Dar es Salaam kuelekea uzinduzi wa Kitabu kitakacho zinduliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa (MB) Aprili 4, 2023 chuoni hapo. Kulia ni Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Geografia, Dkt. Robart Katikilo.
Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Geografia, Dkt. Robart Katikilo akifafanua jambo wakati wa kukielezea kitabu kitakachozinduliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa (MB) Aprili 4, 2023 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Profesa Christine Noe na Kushoto ni Mhadhiri wa Idara ya Geografia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Pilly Siluano.
Mhadhiri wa Idara ya Sosiolojia na Antrolojia, Ndaki ya Sayansi za Jamii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Rechard Sambaiga. akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo Aprili 2, 2023 jijini Dar es Salaam kuelekea uzinduzi wa Kitabu kitakacho zinduliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa (MB) Aprili 4, 2023 chuoni hapo. Katikati ni Mhadhiri kutoka Indara ya Geografia, Faraja Namkesa kushoto ni Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Profesa Christine Noe.
Na Mwandishi wetu, Michuzt TV
UTAFITI unaonyesha kwamba jamii zimepewa majukumu zaidi ya kuhifadhi bila rasilimali za kuziwezesha jamii hizo. Matokeo yake, jamii zimepewa matumaini ya mabadiliko ya kimaisha ambayo hayajawezekana.
Hayo yamesema na Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Profesa Christine Noe kizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 2, 2023 jijini Dar es Salaam kuelekea uzinduzi wa Kitabu cha utafiti kitakachozinduliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa (MB) Aprili 4, 2023 chuoni hapo. Amesema kuwa badala ya jamii kupata matumaini hayo, hifadhi zimepanuka kuelekea ardhi za vijiji, jambo ambalo limesogeza sana mgongano wa matumizi ya ardhi hizo.
Amesema kitabu hicho kimehitimisha kwamba ilitegemewa kwamba ushirikishaji wa jamii katika uhifadhi kungepelekea pia madaraka ya kufanya maamuzi mbalimbali kuhusu maliasili husika.
“Hii imepelekea jamii za vijijini kuendelea kuwa wahanga badala ya wanufaika wa ushirikiano katika kuhifadhi maliasili. Mfano mzuri ni pamoja na wimbi kubwa la ongezeko la wanyamapori maeneo ya vijiji ambalo kimsingi ni matokeo ya kuongezeka kwa ardhi isiyotumika tena kwa shughuli za kibinadamu.”
Amesema Ongezeko la ushirikiano katika shughuli za kuhifadhi maliasili kumeleta matokeo makubwa chanya kwa sekta zote tatu za maliasili. Kimsingi, wingi wa wadau umefanya kuwepo na ongezeko kubwa la maeneo ya misitu (ya nchi kavu na baharini) ambayo pia ni makazi na chanzo cha chakula cha wanyama na samaki.
Amesema kuwa kitabu hicho kimehitimisha kwamba Mabadiliko katika hali ya maisha ya jamii za vijijini (ambazo kwa sehemu kubwa bado ni ya wakulima) yanapatikana pale tu ambapo uzalishaji katika kilimo umeongeza na masoko kupatikana.
“Hii inamaanisha kwamba ushirikishwaji katika shughuli za uhifadhi kumeleta ubora wa sera katika kutoa haki na usawa, ufanisi pamoja na kufungua fursa za biashara, bado uhifadhi haujaweza kuwa tegemeo katika kuleta maendeleo kwa jamii za wakulima. “ Ameeleza
Akizungumzia utofauti uliopo Amesema kuwa Utofauti upo kidogo kwa jamii zinazopakana na hifadhi za misitu kwani sera za misitu zimetoa fursa za uvunaji unaowezesha jamii kuongeza kipato.
“Hii ni kulinganisha na jamii za maeneo ya uvuvi na wanyamapori ambapo vibali vya uvunaji au shughuli mbadala havikufanikiwa ama kuchukuliwa na wawekezaji wachache wakubwa.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...