Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Profesa Christine Noe katikati a akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 2, 2023 jijini Dar es Salaam kuelekea uzinduzi wa Kitabu kitakacho zinduliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa (MB) Aprili 4, 2023 chuoni hapo. Kulia ni Mhadhiri kutoka Idara ya Geografia, Faraja Namkesa na kushoto ni Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Geografia, Dkt. Robart Katikilo.

Na Mwandishi Wetu, Michuzi Tv
SERIKALI imetakiwa kuhakikisha kwamba juhudi za kushirikisha jamii zinakwenda sambamba na kujenga imani kwamba jamii hizo kweli ni wanamiliki wa maliasili na wanaweza kuiamini serikali na wadau wengine.

Hayo yamesema na Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Profesa Christine Noe akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 2, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa taarifa kwa umma juu ya uzinduzi wa kitabu cha utafiti juu ya hoja kinzani inayosema, Je Ongezeko la Ushirikiano wa Wadau katika Uhifadhi wa Maliasili li umeleta Maendeleo Endelevu nchini Tanzania? Amesema kuwa kitabu hicho kimependekeza mambo mbalimbali ikiwa pamoja na kama serikali haishirikisho jamii bado kuna mashaka makubwa kwa wanajamii ni wadau wanufaika wa Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali na wadau mbalimbali.

Serikali kuhakikisha kwamba faida zinazotokana na ushirikiano katika kuhifadhi zinagawanywa kwa usawa kwa wanajamii na kuepuka kufaidisha watu wachache

  •  Kumaliza mgongano au kutokueleweka kwa mgawanyo wa majukumu ya wadau mbalimbali wa uhifadhi vinavyopunguza ufanisi wa malengo ya ushirikiano
  •  Kuwepo malengo ya muda mrefu ya upatikanaji endelevu wa fedha za kugaramia shughuli za uhifadhi.
  • Uchapishwaji wa nakala za tafiti na sera kwa lugha na namna ambayo ujumbe utafikia jamii ili kuwezesha ushiriki katika mabadiliko yanayotakiwa.
  • Serikali na wadau wengine kutoa motisha wa kiuchumi ili kuendelea kusaidia miradi mbalimbali ya kijamii kuleta matokeo chanya ya kimaendeleo.
  • Kadiri jamii inavyozuiwa kutumia maliasili, ni muhimu kwa jamii hizo kuwezeshwa kuanzisha vyanzo mbadala vya Maisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...