Na Mwandishi Wetu
IMEELEZWA kwamba hivi sasa kuna viongozi wengi walioaminiwa na kupewa madaraka ya kutoa haki katika jamii lakini wengine wanasuasua kutoa haki kwa sababu ya kuogopa kufukuzwa kazi.

Kadharika, Watu wengi wameonewa katika maeneo ya kazi, na wengine hata kuhukumiwa bila hatia kwa sababu tu kiongozi fulani analinda maslahi yake

"Tusiwaonee watu kwa kutetea vibarua vyetu,".

Ujumbe huo ulitolewa na Mchungaji Dkt. Daniel John Seni Modereta, Kanisa la Presbyterian Church in Tanzania, Jimbo la Dar es salaam na Pwani (JDP) kwenye Mahubili ya 'Salamu za Pasaka Jijini hapa.

Alisema kuwa Bwana Wetu Yesu Kristo aliteswa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu ambapo jambo hili Mungu alikuwa amelikusudia ili kuwaokoa wanadamu wale wanaomkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao.

Dkt. Seni, alisema hata pamoja na kuwa Mungu alijua kila kitu ambacho kingetokea, bado kuna watu walioshiriki kusulubiwa kwa Yesu bila kuwa na hatia yoyote.

"Wanadamu kama wanadamu wanawajibika kwa matendo yao,

katika Pasaka ya mwaka huu 2023 tumwangazie huyu Liwali au Gavana maarufu kwa jina la Pontio Pilato,; alisema Mchungaji na kuongeza;

"Huyu alikuwa gavana wa tano wa Jimbo la Kirumi la Yudea, akihudumu chini ya Mfalme Tiberio wakati wa Yesu na huyu ndiye aliyesimamia kesi ya Yesu na hatimaye kuamuru asulubiwe,".

Pilato aliamuru Yesu auawe si kwa sababu aliona hatia kwake, bali kwa sababu ya shinikizo la Wayahudi, mara kadhaa Pilato alijaribu kumfungua Yesu, lakini vitisho vilimzuia.

Alisema kuwa tukisoma katika Injili ya Yohana 19:12-13 tunaona kwamba Wayahudi walimtishia Pilato kuwa “Ukimfungua huyu, wewe si rafiki yake Kaisari.” Neno hili lilimwogopesha, kwani alijua wazi kwamba asipotekeleza matakwa yao basi angekosa kibarua au angefukuzwa kazi kwa kusababisha fujo mjini.

Mchungaji Dkt. Daniel, alisema kuwa kwa sababu ya kutetea nafasi yake, ilibidi amhukumu Yesu sawasawa na matakwa ya Wayahudi.

Alisema Pasaka ya mwaka huu itukumbushe kumrudia Bwana na kutenda haki kwa watu wote bila kuogopa mamlaka ya juu yetu kama kiongozi wa juu anavunja sheria na kupotosha haki, kiongozi wa chini anayejitambua na anayemcha Mungu anapaswa kukataa na kukubali gharama za kufukuzwa kazi.

"Naomba nitoe wito kwa viongozi wote kwamba tuacha kuwaonea watu kwa sababu ya uduni wao, au kwa sababu ya watu wachache wenye chuki dhidi yao," alisema

Alisema Pasaka ya mwaka huu itukumbushe kumrudia Bwana na kutenda haki kwa watu wote bila kuogopa mamlaka ya juu yetu, kama kiongozi wa juu anavunja sheria na kupotosha haki, kiongozi wa chini anayejitambua na anayemcha Mungu anapaswa kukataa na kukubali gharama za kufukuzwa kazi.

"Ni wito kwa viongozi wote kuacha kuwaonea watu kwa sababu ya uduni wao, au kwa sababu ya watu wachache wenye chuki dhidi yao na ninawatakiwa Pasaka Njema."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...