WAKALA wa Huduma za Misitu nchini TFS wametoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje kwenda kuwekeza kwenye maeneo yaliyotengwa ndani ya misitu hiyo Kwa ajili ya  shughuli za utali ikolojia.

Utalii huo wa ikolojia ni zao jipya la utalii nchini ambao unafanyika kwa umakini katika maeneo yaliyo hifadhiwa vizuri.  

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mkuu wa sehemu ya kutangaza utalii ikolojia kutoka TFS, Anna Lauo,  kutoka Wilaya ya Kisarawe Mkoani pwani.

Lauo amesema TFS imepandisha hadhi takriban misitu  20 ya asili kuwa Misitu ya Mazingira Asilia (Nature Forest Reserves) ambapo ndani ya misitu hii kuna viumbe  na mi.ea adimu ambavyo havipatikani duniani kote. 

Pia wasanii mbalimbali wametembelea vivutio hivyo ikiwemo kuzunguka mbuyu wa maajabu ambao kadri unavyouzunguka mara nyingi miaka ya kuishi inaongezeka.

Mkuu wa sehemu ya kutangaza utalii ikolojia kutoka TFS Anna Lauo akitoa maelezo ya mti pekee unaopatikana msitu wa Pugu Kazimzumbwi Kwa watalii pichani hawapo waliofika kutembelea hifadhi hiyo.

Wakala wa Huduma za Misitu nchini TFS wametoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje kwenda kuwekeza kwenye maeneo yaliyotengwa ndani ya misitu hiyo Kwa ajili ya  shughuli za utali ikolojia.  Utalii huo wa ikolojia ni zao jipya la utalii nchini ambao unafanyika kwa umakini katika maeneo yaliyo hifadhiwa vizuri. 

Akizungumza wilayani Kisarawe Mkoani pwani   Anna Lawuo, Mkuu wa Sehemu ya kutangaza Utalii ikolojia TFS,  amesema TFS imepandisha hadhi takriban misitu  20 ya asili kuwa Misitu ya Mazingira Asilia (Nature Forest Reserves) ambapo ndani ya misitu hii kuna viumbe  na mimea isiyopatikana mahali kwingine duniani
Baadhi ya watalii wakifurahia mazingira mazuri ndani ya hifadhi ya misitu huku wakala wa huduma za misitu nchini TFS wakihamasisha wawekezaji kwenda kuwekeza Kwa maeneo yaliyotengwa ndani ya misitu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...