Naibu waziri, ofisi ya waziri mkuu - kazi, vijana, ajira na wenye enye ulemavu Patrobas Katambi amewataka Waajiliwa wa sekta binafsi na sekta isiyo Rasmi hasa wajasiriamali kujiunga na mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) ili kujiwekea akiba Kupata fursa mbalimbali za kiuchumi zinazoratibiwa na mfuko huo.

Naibu waziri Katambi ameyasema hayo kwenye maonyesho ya maadhimisho ya siku ya kitaifa ya usalama mahala pa kazi, Mjini Morogoro yalioratibiwa na Wakala wa usalama na afya mahala pa kazi (OSHA).

Akizungumza alipotembelea banda la mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii NSSF kujionea namna mfuko huo unavotekeleza majukumu yake ya usalama na afya mahala pa kazi amesema ni vyema watanzania Wote wenye sifa za kujiunga na mfuko huo wajiunge.

Aidha Naibu waziri Katambi amepongeza jitihada za NSSF kwa kuboresha huduma kwa Kutoa huduma kimtandao hali inayowalaishia wateja wake Kupata Taarifa wakati wowote.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...