Muonekano wa zahanati ya Mwanalugali A, Halmashauri ya Mji Kibaha,Pwani iliyojengwa kwa ufadhili wa TASAF ,ambayo ujenzi wake imekamilika kwa kwa asilimia 95

UJENZI wa mradi wa Zahanati ya Mwanalugali A Kibaha Mjini unaofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF itakayowahudhumia wakati 3367 umefikia asilimia 95

Katika kufanikisha ujenzi wa mradi huo,jumla ya wananchi 1009 wamejitokeza kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kutoa nguvukazi ili kupunguza gharama za ujenzi na kuharakisha ukamilishaji ambapo jumla ya Shilingi 22,000,000 zimeokolewa kwa nguvukazi yao

Mratibu wa TASAF Kibaha Mjini Anitha Lyoka amesema kando ya kufikia 95% mradi haujanza kutumika kwani fedha za ujenzi zimeisha

"Fedha ya ujenzi imeisha na ujenzi bado haujafikia 100%,taratibu za kuomba fedha kutoka TASAF makao makuu kwa ajili ya ukamilishaji zinaendelea"ameongeza

Diwani wa Kata ya Tumbi kwenye Mtaa Mtaa wenye mradi Mhe.Raymond Chokala ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa mradi huo unaolenga kuimarisha afya za Wananchi na kuwa huo ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde amesema yeye kama msimamizi wa Halmashauri anaendelea kutekeleza wajibu wake kuhakikisha thamani ya fedha inaendana na ubora wa miundombinu inayotekelezwa

Gharama ya mradi ni shilingi milioni 113,964,285 kati ya fedha hizo TASAF imetoa shilingi 91,964,285 na mchango wa Jamii ni shilingi 22,000,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...