Kulia ni Frola Mgonja Ofisa Tawala Mwandamzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala akizindua Ripoti ya mwaka 2023 ya Stadi za maisha na maadili jijini Dar es Salaam Mei 12, 2023. kushoto ni Omari Ngalomba Mkurugenzi wa Shirika la Galuka Kwalala Youth and Enviroment.
Frola Mgonja Ofisa Tawala Mwandamzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala akionesha Ripoti ya mwaka 2023 ya Stadi za maisha na maadili jijini Dar es Salaam Mei 12, 2023. 
Elizabeth Lazoro mmoja wa Wanafunzi waliohusishwa kwenye utafiti wa Stadi za Maisha na Maadili akieleza namna utafiti huo ulivyomuwezesha kukua kifikra.
Frola Mgonja Ofisa Tawala Mwandamzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala akizungumza mara baada ya kuzindua Ripoti ya mwaka 2023 ya Stadi za maisha na maadili jijini Dar es Salaam Mei 12, 2023. kushoto ni Omari Ngalomba Mkurugenzi wa Shirika la Galuka Kwalala Youth and Enviroment.
Hasna Kingu Mmoja wa watatifiti wa Ripoti ya Stadi za maisha na Mkufunzi kutoka taasisi ya Milele Zanzibar foundation akiwasilisha sehemu ya ripoti hiyo kabla ya kuzinduliwa.
Gloriana Msengi Mwakilishi wa Ofisa Elimu jiji la Dar es salaam akizungumzia ripoti ya Stadi za Maisha.



SERIKALI imeipungza ripoti ya utafiti wa stadi za maisha na maadili kutokana na kutoa taswira ya kupunguza ukatii kwa watoto nchini.

Frola Mgonja Ofisa Tawala Mwandamizi wa Wilaya ya Ilala aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogoro kwenye uzinduzi wa Ripoti hiyo uliofanyika leo tarehe 12 Mei, 2023 Gongolamboto jijini Dar es Salaam, amesema kuwa ripoti hiyo imejibu maswali ambayo viongozi wa Serikali walikuwa wakiiumiza vichwa juu ya masuala ya watoto.

Ripoti hiyo imeandaliwa na tasisi ya Milele Zanzibar Foundation, Zizi Afrique Foundation, UDSM, Uwezo Tanzania, Girls Livehood, Reginal Education Learning Initiative na Gulaka Kwalala Youth and Enviroment Group.

Amesema kuwa ripoti hiyo itachochea kupunguza ukatili wa watoto kwa kuwa imeeleza na watoto walivyopewa ujasiri wa kujitambua na kuwa na uwezo wa kujieleza.

"Watoto wakiwa na uwezo wa kijieleza kwa asilimia kubwa changamoto ya ukatii kwa watoto wetu itakoma", amesema Frola.

Ofisa Mwandamizi wa Serikali huyo amesema kuwa yaliyowasilishwa kwenye ripoti hiyo yachukuliwe na watunga sera lakini pia yasiishie kwenye machapisho yafanyiwe kazi kwa nchi nzima.

Omari Ngalomba Mkurugenzi wa Shirika la Guluka Kwalala Youth and Enviroment Group shirika ambalo limekuwa kinara wa uandaji wa ripoti hiyo amesema kuwa ripoti hiyo imeakisi mazingira halisi ya mtaani ambapo wawakilishi wa mashirika hayo walifanya utafiti.

George Pius Mratibu wa mradi huo wakati anawasilisha sehemu ya ripoti hiyo, amesema kuwa ripoti hiyo ni utafiti uliofanywa kwenyekaya 336 maeneo 20 kwenye Wilaya ya Ilala ambapo imetathimin vijana wa kuanzia miaka 13 mpaka 17.

Amesema kuwa ripoti hiyo imebaini kuwa asilimia 41 ya wanauwezo kuwepo kwa tatizo kwa mtanzamo mmoja na kuchukua hatua juu ya suala hilo .

"Tathamin imewapima vijana na kubaini kuwa asilimia 30 hawewezi kufanya matumizi ya simu za kidigitali na 33 wanatumia kirahisi huku asilimia 37 wanatumia kwa tabu" amesema Pius .

Naye Hasna Kingu mwakilishi wa stadi , maisha kupitia mpango wa 'Alive' amesema kuwa tathimin ya ripoti hiyo imefanywa na tasisi ya Milele Zanzibar Foundation, Zizi Afrique Foundation, UDSM, Uwezo Tanzania, Girls Livehood, Reginal Education Learning Initiative na Gulaka Kwalala Youth and Enviroment Group.

Hasna ametanabaisha kuwa utafiti huo umefanywa kwenye wilaya 34 za Tanzania Bara ambapo ulilenga kubaini uwezo wa watoto kwenye saikolojia, hisia, akili, na maadili.

"Ripoti hii imepima maadili, heshima, uwezo wa kusoma, kutumia digitali na kujitambua" alisema Hasna.

Diwani wa Gongolamboto Lucas Rutainurwa, amesema kuwa kuwa Tathimin hiyo iingie kwenye utekelezaji kwa vijana "Sisi tunaona kuwa ni vema yaliyoelezwa kwenye ripori yaingizwe kwenye mitaala katika shule"

Amesema kuwa ripoti hiyo imemshawishi kuipigia chepuo "Sisi kama watunga sera ripoti hii tutaichukua ili kwenda kufanyiwa kazi" alisema.

Amesema kuwa mafunzo yayopatikana kwenye tathimini hiyo yasaidie kwenye maadili.

Gloriana Msengi Mwakilishi wa Ofisa Elimu Jiji la Dar es Salaan amesema kuwa ripoti hiyo imebeba mambo muhimu na kwamba ingefaa kuwa sehemu ya somo kwenye mitaala ya shule nchini.

Kuhusu suala la mmonyoko wa maadili, amesema kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa mstari wa mbele kuharibu maadili "tunaona kuna ombwe kwenye jamii kuna kazi kubwa kwenye jamii muhimu kuwe na elimu kwenye jamii ili mtoto asaidiwe kutimiza ndoto zake"

Msengi amesema kuwa watoto wakisharejea shuleni nyumbani anakutana na changamoto ya kujielea wenyewe wazazi wapo bize na mambo yao .

Naye Elizabeth Lazoro mwanafunzi amesema kuwa stadi hiyo ya kupima uwezo imemsaidia kifikra na kumuongezea uwezo wa kijiamini kwenye utatuzi wa matatizo.

"Nimesaidia kuwa na uwezo wa kijitathimin kujitambua na kuwa na uwezo wa kutatua matatizo yangu binafsi",amesema Elizabeth.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...