Wananchi wakionesha utaratibu wa uzimaji moto kwa vyombo vinavyotumia mafuta wakati wa utoaji wa elimu kwa wananchi wa Bagamoyo kuhusiana usalama vyombo vya usafiri majini.*Yaunganisha nguvu ya usalama majini kwa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji pamoja na NEMC

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Bagamoyo
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeendelea kutoa elimu kwa wananchi wa mji mdogo wa Bagamoyo juu ya usalama kwa wanapotumia vyombo vya usafiri majini.

Utoaji wa elimu ya usalama wa usafiri wa vyombo vidogo majini uliotolewa na TASAC umeambatana na vyombo vingine vya serikali ambao ni Jeshi la Zima Moto na Uoakoji pamoja na Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC).

Akizungumza wakati wa utoaji elimu ya usalama Majini Nahodha Alex Katama, Mkaguzi wa vyombo vya usafiri Majini na Msimamizi wa Kituo cha Utafutaji na Uratibu wa Uokoaji kutoka TASAC, amesema TASAC iko katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama wanavyotumia vyombo vya usafiri majini.

Katama amesema vyombo vya usafiri majini vinatakiwa kukaguliwa kabla ya kuanza safari iwe ya Uvuvi au kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Aidha, amesema kuwa mabaharia wanapochukua vyombo vya majini wahakikishe vifaa vya usalama vipo na ikitokea vifaa hivyo havipo basi safari inayotakiwa kufanyika iahirishwe.

"Haiwezekani mtu ananunue mtumbwi milioni 10 lakini inatokea anashindwa kununua jacket la uokozi na vifaa vingine ambavyo havifiki laki Tano hapo ni tatizo hivyo watu watimize wajibu wao wa matakwa ya kisheria" amesema Katama.

Afisa wa Ukaguzi wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji SSGT Mganga Mkama amesema kuwa baadhi ya watu wana vifaa vya zimamoto lakini hawajui kuvitumia hivyo kila mmoja kwenye mitumbwi wawe na vifaa hivyo na waweze kuvitumia.

Amesema kuwa mitumbwi yote katika kuwa salama wanatakiwa kuwa na vifaa kinga pale panapotokea janga la moto kuweza kusaidia kujiokoa au kuzima moto huo.

Mkama amesema kuwa TASAC imekuja kutoa elimu ambapo kwa Jeshi la Zima Moto na uokoaji inashirikiana nao kuendelea kutoa elimu hiyo kutokana kuwa majini kuna rasilimali na kiteoe ambavyo kuvipata inabidi usafiri wa vyombo vya usafiri wa majini.

Meneja wa Baraza la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) Ndimbumi Joram amesema usalama wa usafiri unatakiwa kwenda na uhifadhi wa mazingira hivyo ni marufuku kutumia mifuko ya rambo na kutupa takataka hovyo kwenye fukwe za bahari.

Amesema kuwa kama kuna watu wanaoleta mifuko ya rambo na vifungashio vingine waache mara moja kwani wanaharibu mazingira ya bahari.

Ukitunza mazingira yatasaidia shughuli za uvuvi kuendelea na kuwa endelevu.
Nahodha wa Usimamizi wa Majini wa Kituo cha Utafutaji na Uokoaji wa Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) Alex Katama akizungumza na wananchi wa Bagamoyo (Hawapo pichani) kuhusiana  namna ya kutumia vyombo vya usafiri wa majini kwa kuzingatia usalama.
Ufisa Ukaguzi Jeshi la Zimamoto SSGT  Mganga Mkama akitoa maelezo kuhusiana na matumizi ya vifaa vya Zima Moto kwa vyombo vya Usafiri Majini wakati utoaji wa elimu kwa wananchi Bagamoyo iliyoratibiwa na TASAC.
Meneja wa Kanda ya Bagamoyo  wa Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira Ndimbumi Joram akizungumza kuhusiana utunzaji wa mazingira ya Bahari wakati utoaji wa elimu kwa wananchi juu usalama wa utumiaji wa vyombo vya majini.
Afisa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa TASAC  Nicholaus Kinyariri akitoa maelezo juu umuhimu wa kuzingatia  mambo muhimu ya usalama kwa vyombo vya usafiri majini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...