Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
KONGAMANO la siku mbili la mjadala wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia lililobeba azma iliyotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhamasisha nishati safi ya kupikia ili kumuondolea adha mwanamke wa kitanzania kwenda kutafuta kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia limemalizika leo jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo limewahusisha wanawake kutoka Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam na limeandaliwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TABWA) ambapo pamoja na kutolewa mada mbalimbali washiriki wapatao 200 wamepatiwa mitungi ya gesi ya Oryx kama sehemu ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa.
Akizungumza kwenye kongamano hilo ambalo limeshirikisha washiriki 200, Mkurugenzi wa TABWA Noreen Mawalla amesema wanatambua juhudi za Serikali katika kuhakikisha mwanamke wa Tanzania anaondolewa changamoto zinazomkabili na matumizi ya kuni na mkaa yamesababisha wanawake kutumia muda mwingi kusanya kuni.
"TABWA tumefurahishwa na muitikio mkubwa wa wafanyabiashara waliojitokeza katika kongamano hili na tumewasikia walivyokuwa wanaelezea umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia, wamesikiliza mada na wamepata nafasi ya kuuliza maswali na kujibiwa, " amesema.
Aidha amesema baada ya Dar es Salaam na Pwani kongamano kama hilo litafanyika kwenye Mkoa ya Mtwara, Lindi, Morogoro, Dodoma, Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Iringa, Njombe, Mbeya,Songwe na Rukwa.
"Tumepanga kutoa elimu, kupanga mikakati ya utekelezaji na kujenga mtandao wa biashara kwa ujumla "amesema Mawalla huku akifafanua kongamano hilo limewahusisha zaidi wanawake, vijana, wauza mkaa, watengenezaji na wauzaji wa majiko ya nishati safi.
"Pia tulikuwa na wamiliki wa migahawa, shule, hoteli, vyuo,wataalamu wa afya na mazingira pamoja na wadau wengine wote tunawakaribisha ili waje wapate elimu na kujenga mtandao wa kibiashara kupitia nishati safi ya kupikia"amesema.
Kuhusu mitungi ya Oryx ambayo imetolewa kwa washiriki Mawalla amesema anaishukuru kampuni ya Oryx kwa kutoa mitungi hiyo kwani imedhihirisha kwa vitendo wanaunga mkono kile ambacho wanakifanya katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx, Peter Ndomba, amesema kuwa hivi sasa watumiaji wa nishati safi ya kupikia ni asilimia tano tu huku lengo la Serikali ni kufikisha watumiaji zaidi ya asilimia 80 kwa miaka kumi ijayo, hivyo wadau wanayo nafasi ya kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati ya gesi .
"Mpaka sasa watumiaji wa nishati safi ya kupikia ikiwemo gesi ni asilimia tano tu ambayo bado ni hafifu huku lengo la Serikali ni kufikisha watumiaji zaidi ya asili 80 Kwa miaka kumi ijayo.Wakati umefika sasa wa kuunga mkono jitihada za Serikali za kupambana na matumizi ya kuni na mkaa ili kudhibitibi uharibifu wa mazingira unaochangia mabadiliko ya tabia nchi.
"Katika jitihada zetu za kuiunga mkono Serikali ya kumtua mama kuni kichwani, tumetoa gawa bure mitungi ya gesi zaidi ya 7,000 katika kipindi cha mwaka mmoja na leo hii tumegawa mitungi 200 kwa wajasiriamali ambao wameshiriki kongamano hili na tutaendelea kugawa kwa makundi mengine, amesema.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx Peters Ndomba akielezea kwenye kongamano.
Sehemu ya anawake wajasiriamali kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambao wameshiriki Kongamano lililohusu Nishati Safi ya kupikia lililoandaliwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania(TABWA)wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa mitungi ya majiko ya ORYX jijini Dar es Salaam
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa TABWA Noreen Mawalla katikati Mheshimiwa Diwani wa Bagamoyo Shumina Sharifu akipokea jiko kwa Nisahati Safi kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx Gas Peter.
Wapili kutoka kushoto ni Mheshimiwa Diwani Bagamoyo Shumina Sharifu, Mkurugenzi TABWA Noreen Mawalla, Mwanaisha Kikwete na Khdija Makamba wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika.kwa Kongamano hilo.(Picha Zote na Said Mwinshehe)




.jpeg)

.jpeg)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...