Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Viongozi wafuatao kuwa na Hadhi ya Balozi kama ifuatavyo:-
Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi kuwa Balozi;
Dkt. Salim Othman Hamad, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia masuala ya Siasa kuwa Balozi; na
Dkt. Kassim Mohamed Khamis, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia masuala ya Hotuba kuwa Balozi.
Uteuzi huu wa Hadhi ya Balozi umeanza tarehe 12 Juni, 2023.
Aidha, Vyeo walivyonavyo vinabaki kama vilivyo.
Wateule wataapishwa tarehe 16 Juni, 2023 kuanzia saa 04:00 asubuhi - Ikulu, Chamwino - Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...