
.jpeg)

TAASISI ya Centre to Advance Research on Health in Africa (CAReH Africa), imetoa msaada wa makoti ya kuvaa madaktari wanapokuwa kazini kwa kituo cha Afya cha Ifakara ambayo yatagawiwa katika hospitali mbalimbali na vituo vya afya nchini.
Akiongea katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika jijini Dar e Salaam hivi karibuni, Mwanzilishi wa taasisi hiyo,Profesa Gbenga Ogedebde, ambaye ni mhadhiri katika chuo Kikuu cha Tiba cha Grossman kilichopo Newyork nchini Marekani, alisema msaada huo ni moja ya mkakati wa taasisi hiyo ya kupambana na changamoto nyingi zilizopo katika sekta ya Afya barani Afrika.
Profesa Ogedebde alisema, CAReH Africa, imejipanga kuhakikisha inawezesha kufanyika tafiti za magonjwa barani Afrika sambamba na kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali kupunguza changamoto nyingi za magonjwa.
“Barani Africa kuna changamoto nyingi katika sekta ya afya,hivyo ni jukumu letu wataalamu wa fani mbalimbali kupambana kwa ajili ya kuzitafutia changamoto,husuani uwepo wa magonjwa mbalimbali yanayopaswa kufanyiwa utafiti kwa ajili ya kukabiliana nayo sambamba na uhaba wa upungufu wa vifaa tiba vya kisasa na matumizi ya teknolojia za kisaa katika kutoa huduma za matibabu.
Kwa upande wake,Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Afya na utafiti cha Ifakara,Dk.Jerry Hella, alishukuru kwa msaada huo na kuongeza kuwa yatagawiwa katika hospitali mbalimbali za hapa nchini.
“Msaada huu umepitia kwetu kwa kuwa tunafanya kazi kwa ushirikiano na taasisi ya CAReH Africa, ila tutayatoa kwa hospitali za Temeke na Mwananyamala.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...