Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akitoa  tuzo kwa wasaidizi wa kisheria ambao walikuwa mstari wa mbele kutoa huduma za kisheria.

RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi ameahidi kutoa majengo ya ofisi pamoja na usafiri wa bajaji kwa watoa huduma za msaada wa kisheria Zanzibar ili kuwawezesha kuwafikia wananchi wengi wanaohitaji huduma hiyo.

Rais Mwinyi ametoa kauli hiyo hiyo jana Jumaimosi, 22 Julai 2023 kwenye kilele cha maadhimisho ya nne ya wiki ya msaada wa kisheria yaliyofanyika katika ukumbi wa Idrissa Abdul Wakili, Kikwajuni, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema serikali yake inakwenda kuchukua hatua hiyo haraka kutokana na ukweli kuwa huduma za msaada wa kisheria ni kiungo muhimu cha upatikanaji wa haki nchini hasa kwa wananchi wasio na uwezo wa fedha pindi wanapohitaji msaada wa kisheria.

"Nimeelezwa hapa kuwa wasaidizi wa kisheria wanahitaji majengo ya ofisi kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli zao vizuri. Lakini pia wanaomba usafiri wa bajaji, hawa watu hawana makubwa pengine wangetaka kuomba magari," amesema Rais Mwinyi na kuongeza:

"Hivyo, mie nalichukua na Serikali inakwenda kulishughulikia haraka. Najua tuna mambo mengi lakini ni muhimu sana kwa ajili ya kujenga mazingira bora ya wao kutekeleza majukumu yao.”

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Legal Service Facility (LSF), Jaji Mstaafu, Robert Makaramba, amesema wasaidizi wa kisheria ni nyenzo muhimu katika kuzisaidia Serikali kuboresha sekta hiyo.

"Suala hili linaanza na uboreshaji wa mifumo, miundo, sera na sheria zitakazohakikisha huduma za msaada wa kisheria zinatolewa katika hali endelevu kupitia uwezeshaji wa Serikali kwa kushirikiana na watoa msaada wa kisheria," amesema Jaji Makaramba.

Hata hivyo ikumbukwe kwamba maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar 2023 yametamatika Julai 22, 2023, ambapo pamoja na mambo mengine Rais Mwinyi alihitimisha kwa kukabidhi tuzo kwa wasaidizi wa kisheria kwa walikuwa mstari wa mbele kutoa huduma za kisheria.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akitoa hotuba yake wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Zanzibar 2023.
Baadhi ya Wajumbe wa Legal Services Facility (LSF) pamoja na Wawakilishi wa Sekretarieti ya LSF wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu iliyoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Zanzibar 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...