Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya uwakala wa vyuo vikuu nje ya nchi (Global Education Link), Abdulmalik Mollel (kulia) akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga wakati wa kufunga Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyomalizika Julai 22, 2023 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya uwakala wa vyuo vikuu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya uwakala wa vyuo vikuu.
TAASISI ya uwakala wa vyuo vikuu vya nje ya Nchi Global Education Link imesema itamboresha mtanzania kupitia mifumo ya ufundishaji na kuondoa changamoto za wanafunzi ambao wanatoka Tanzania kwenda kusoma kwenye nje ya Nchi.
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya uwakala wa vyuo vikuu nje ya Nchi Global Education Link, Abdulmalik Mollel ameyasema hayo wakati wa kufunga Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Julai 17 na kumalizika Julai 22, 2023 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Amesema wamezingatia suala la kuwapa udahili wanafunzi kulingana na gharama wanazotaka wenyewe, yaani kama mtu ana uwezo wa milioni tatu basi anapewa Chuo cha garama hiyo na yule wa milioni 20 nae anapata Chuo kutokana na uwezo wake ma hivyo kuondoa changamoto ya wanafunzi ambao wanatoka Tanzania kwenda kwenye vyuo vikuu vya nje ya Nchi.
Amesema, lengo kubwa la wao kuendelea kusaidia wanafunzi wa elimu ya juu ni kuhakikisha wanamboresha mtanzania yeyote kupitia mifumo ya ufundishaji katika elimu ya juu ili kuhakikisha kile anachojifunza kinakuja kuwa na mantiki kwa nchi yetu.
"Kwa hiyo vyuo vikuu vya nje (development country) tukiunganisha na vyuo vikuu vya kwetu, hawa wakifanya kazi kwa pamoja maana yake tutakuwa na uhakika kuwa yale tunayoyaona kwao kama Maendeleo basi na sisi ndio tunayahitaji, Kama wao wanatengeneza solar sisi tunaagiza solar hivyo tunategemea watengenezaji wa solar kupitia vyuo vikuu basi na sisi vyuo vikuu vyetu vinaweza vikatengeneza solar bila kupitia Muunganiko wa vyuo vyeti vya ndani na vya nje kwani tutakuwa hatuna tatizo la wataalamu wetu" amesema Mollel
Aidha amesema katika maonesho hayo vyuo vikuu vya hapa nchini vyenyewe kwa vyenyewe na vile vya nje vimeweza kukutana na kufanya mazungumzo ya moja kwa moja ili kuongezeana uelewa na namna ya ufundishaji elimu ya juu.
Wito, maonesha ndio mwanzo kwa maonesho mengine. Baada ya maonesho haya kuanzia j.3 tunaendelea na udahili ofisini kwetu ili mtanzania ambaye hukubahatika kuja viwanjani hapa ama.hukupata maamuzi baso njoo ofisini tuweze kukupatia udahili.
Aidha Mollel amesema mpaka sasa maombi wa wanafunzi watanzani 43, waliokuwa wakisoma nchini Sudan na masomo yao sasa yamesimama yanafanyiwa kazi kwa ajili ya wao kuendelea na masomo pale walipoishia.
"Nimekwisha kubaliana na baadhi ya vyuo kwamba mwanafunzi wangu kutoka Tanzania ambae alikuwa anasoma Sudan na amerudi Tanzania, hawana suala la kusema tutamchukua ama hatutamchukua, ni lazima wamchukue la sivyo basi hakuna umuhimu wa kuwa na Muungano sababu hawa wanafunzi wanahitaji msaada mkubwa sana wamekwisha anza wako katikati ya masomo halafu wamekwama" amesema Mollel
Amevitaja vyuo vikuu wanavyoshirikina navyo kwenye maonesho hayo ni pamoja na vyuo vikuu vya UK,Vyuo vikuu vya Canada,vyuo vikuu vya India, Australia,Sypris,Mauricius,Uturuki,Malaysia na Nchi nyingine mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...