DC Matinyi akiwa katika pichaya pamoja na walinufaika na mikopo ya 10% ambayo imewawezesha kukuza biashara zao.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mobhare Matinyi akiangalia bidhaa mojawapo ya wajasiriamali ambayo imesindikwa katika moja ya banda kwenye maonesho ya Biashara Kimataifa yaliyofikia kileke leo Mkoani Dar es Salaam.DC Mobhare Matinyi akiangalia kitenge aina ya Batiki.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mobhare Matinyi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea katika Banda la Manispaa ya Temeke leo.
Na Khadija Kalili
MKUU wa Wilaya ya Temeke Mobhare Matinyi amewashauri wajasiriamali waliowezeshwa kwa kupata mikopo ya asilimia 10 kuboresha bidhaa zao ili ziweze kuleta ushindani katika Soko la Kimataifa.
Ameyasema hayo leo Julai 07, 2023 wakati wa kutembelea Banda la Manispaa ya Temeke katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayioendelea kufanyika katika viwanja vya SabaSaba jijini Dar es Salaam. Ametembelea na kukagua huduma mbalimbali zinazotolewa na banda la Manispaa ya Temeke.
"Nimefurahi kuona vikundi hivi vya wajasiriamali wakiwa na bidhaa zao, lakini changamoto kubwa si kwa vikundi hivi tu vya Temeke bali kwa nchi nzima kuweza kuboresha bidhaa zao kwa ajili ya kuzipandisha thamani na kuweza kuketa ushindani wa Soko la ndani na nje ya nchi....tuna soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki tunaweza kuuza bidhaa zetu huko katika nchi zaidi ya sita." Amesema DC Matinyi
Wakati huo huo Mkuu huyo wa Wilaya aezungumzia kuhusu suala la uvamizi wa maeneo ya wazi na kuitaka Idara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuweka matangazo katika maeneo hayo ili kuepuka watu kuyavamia.
Maonesho ya Biashara Kimataifa (SabaSaba) yameanza rasmi Juni 28 mwaka huu na yanatarajiwa kufungwa Julai 13,2023 ambapo Manispaa ya Temeke inashiriki Maonesho haya kwa kusogeza huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo huduma za utoaji wa leseni mbalimbali, huduma za Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa(ICHF) na nyinginezo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...