Na. Damian Kunambi, Njombe.

Wakazi wa kata ya Mavanga wilayani Ludewa mkoani Njombe, wametuma salamu za pongezi na Shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumsikiliza mbunge wao Joseph kamonga na kutoa fedha za miradi mbalimbali ya kimaendeleo wilayani humo na hasa katika kata hiyo ya Mavanga.

Wananchi hao wametoa pongezi hizo mbele ya mbunge huyo mara baada ya kuwasili katani hapo akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wa chama cha Mapinduzi pamoja na wakuu wa idara mbalimbali na kufanya mikutano ya hadhara katika vijiji vya kata hiyo.

Patrick Mtega ni miongoni mwa wananchi hao amesema ana imani kubwa na Rais Dkt. Samia pamoja na mbunge huyo kwani kwa kipindi kifupi cha uongozi wao wameshuhudia fedha za miradi kama maji, shule, mabweni ya wanafunzi, vyumba vya madasa na barabara zikiletwa katani humo.

"Kwakweli mimi si mtu wa kupindisha pindisha maneno, huyu mbunge kwa mara ya kwanza nilimuona kwenye picha ya bango akigombea nafasi ya ubunge. Yaani kitendo cha kuiona tuu picha akili yangu ikaniambia huyu anafaa na nimchapa kazi, sasa leo nimehakikisha hilo". Amesema Mtega.

Kata hiyo imepokea fedha za mradi wa maji katika kijiji cha Mavanga kiasi cha sh. Bil. 1.5, mradi wa ujenzi wa shule ya msingi kitongoji cha Ruhuhu getini Mil. 347.5, kuboresha shule ya msingi Mbugani na matundu ya vyoo Mil. 81 pamoja na ujenzi wa bweni la wanafunzi Mil. 130 huku miradi mingineyo ikiwa katika mchakato wa kupatiwa fedha.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...