Na Jane Edward, Arusha
NAIBU waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Matthew Kundo amelitaka Shirika la Posta Tanzania kuendana na kasi ya utoaji wa huduma kidigitali na kwamba Serikali imeshaanza jitihada za kuweka WiFi kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza jijini Arusha wakati akifungua kikao cha 41 cha Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) kinachoendelea jijini hapa, Mhandisi Kundo amesema Serikali inajipanga kuimarisha huduma za mawasiliano nchini.

Ameongeza huduma hizo ni pamoja na kuweka mtandao wa Intaneti wa bure (WiFI) kwenye mikusanyiko yote, vyombo vya usafiri na kwenye shule, ili kila mwananchi apate huduma hiyo bila usumbufu wowote.

Amesema uwekaji huo wa Intaneti za bure, zitasaidia wananchi kupata huduma za mawasiliano popote wanapokuwa na kuendelea na shughuli zao za kijamii, bila mkwamo wa ukosefu wa huduma hiyo.

“Serikali ya awamu ya sita imejipanga, tunataka kuhakikisha umoja huu na wenzetu unaboresha mifumo ya utendaji kazi na kua ya kidijitali na sisi kama Tanzania tukiwa wanachama wa umoja huu Afrika na Duniani, tumeanza mikakati,"amesema.

Ameongeza miongoni mwa makubaliano yaliyowekwa na Umoja wa Posta Afrika ni pamoja na kuboresha miundo mbinu yetu ya Mawasiliano kwa kuweka sawa sera yetu ya posta ya mwaka 2003, ”amesema

Amefafanua mojawapo ya maboresho hayo ni ujenzi wa minara, mkongo wa Taifa na uwekaji wa Anuani za Makazi, ili kuhakikisha shughuli zote za posta zinafanyika vizuri na wananchi wanapata huduma za kijamii bila usumbufu.

Aidha amesema Rais Samia Hassan Suluhu Februari 8 , 2023 alihakikisha Tanzania kunakuwa na Anwani za makazi na hilo lilifanyika kwa ufanisi, ambapo kwa sasa kila mmoja anaona faida yake katika upatikanaji wahuduma za kijamii na hata posta inakua rahisi.

“Tunavyoelekea kutoa huduma zote kidijitali ni lazima kuhakikisha uwezo wetu kimtandao unakua imara ili ifike kila mahali, kila mmoja asione umuhimu wa kutembea na fedha tasilimu, bali kadi tu na kupata kila aina ya huduma mtu anayohitaji kupata,”amesema

Awali Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la PAPU, Richard Ranarison, amesema umoja huo unakusudia kutoa huduma bora na kwa wakati kwa kila nchi na ili kufikia lengo hilo, kila wanapokutana kwenye vikao vyao vya kila mwaka wanaangalia wapi walipo na wanapoelekea na penye dosari wanazirekebisha.

Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni mfululizo wa vikao kwa ajili ya kuandaa ajenda ya pamoja kwa nchi za Afrika ili kuziwasilisha katika kikao cha Baraza la Posta Duniani kitakachofanyika Oktoba mwaka huu.
Naibu waziri wa habari, mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Matthew Kundo akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
 Dkt. Sifundo Chief Moyo mtendaji Mkuu wa Posta Afrika akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...