Na Nasra Ismail, Geita
JUMLA ya Sh. millioni 60 zimetengwa katika bajeti ya mwaka huu kwa ajili ya kumalizia nyumba za walimu pamoja na vymba vya maabara katika shule za sekondari zilizopo nje ya mji ambazo zinapatikana katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mji.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya elimu ya Kata mbalimbali wilayani humo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani Ofisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Geita Mji Rashid Mhaya amesema kumekuwepo na changamoto mbalimbali kwenye sekta ya elim ambazo zinaendelea kutatuliwa taratibu.

Amezitaja changamoto hizo ni ukosefu wa uzio katika shule ya sekondari Kasamwa kwa ajili ya usalama wa wanafunzi katika sekondari hiyo ya bweni, upungufu wa nyumba za walimu pamoja na vymba vya maabara.

"Ni kweli kwamba shule zetu nyingi za pembezoni zina mahitaji makubwa ya nyumba za walimu na hii ni kwasababu wanahitaji kuwa karibu ili waweze kupata utulivu utendaji kazi wao" amesema Mhaya.

Pia amesema kipaumbele cha kwanza kwa sasa ni ujenzi wa shule ya sekondari Ibanda itakayojengwa Kata ya Kanyara kwani wanafunzi wanaoishi katika kata hiyo wanatembea umbali wa kilometa 20 kuifata shule ya Kasamwa.

"Tulisha ahidi katika eneo hili kwamba Ibanda sekondari ni kipaombele cha kwanza kutokana na wanafunzi kutembea umbali mrefu, kilometa 20 kufatwa elimu kusema ukweli inachosha, " amesema Mhaya.

Kwa upande wao madiwani wamepongeza hatua hiyo ni kuahidi kuunga mkono huku wakipongeza jitihada zinazofanywa na maofisa elimu sekondari na msingi kwani kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye sekta ya elimu katika wilaya ya Geita Mji.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...