
RAIS Samia ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa mkongo wa mawasiliano wa 2Afrika na matumizi ya teknolojia ya 5G iliyofanyika katika ofisi za kampuni ya Airtel zilizopo Tanki Bovu.
Aidha, Rais Samia amesema misingi imara kwenye TEHAMA na mifumo ya mawasiliano kisera, kisheria na kitaasisi itawezesha kujenga uchumi jumuishi wa kidijitali (Digital Inclusive Economy) na kuinua maisha ya wananchi mijini na vijijini.
Vile vile, Rais Samia amesema uzinduzi wa teknolojia ya 5G itarahisisha utoaji wa huduma mbalimbali, ikiwemo utunzaji taarifa muhimu, ukusanyaji maduhuli ya serikali, kutuma na kupokea fedha pamoja na biashara za mitandaoni.
Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema kuongezeka kwa mkongo huu kutatoa fursa kwa mitandao ya simu na watoa huduma wengine kuchagua mkongo wanaotaka kutumia, hivyo kuongeza ubora na kushusha gharama za intaneti.
Mkongo wa 2Afrika unaunganisha bara la Asia, Ulaya na Afrika kwa urefu wa kilometa 45,000 na kutumiwa na zaidi ya watu bilioni 3 duniani.
Serikali imeanza mradi wa ujenzi wa minara mipya 758 kwa ajili ya kupanua wigo wa mawasiliano (coverage) itakayowanufaisha Watanzania zaidi ya milioni 8 kote nchini na kupunguza gharama za kuweka mkongo kwenye hifadhi za barabara.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...