Na Said Mwishehe, Michuzi TV

RAIS wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muunga wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya ICT na teknolojia hayaepukiki katika sekta ya kilimo kwa karne ya sasa huku akieleze jinsi inavyotumika nchini katika sekta hiyo.

Akizungumza leo Septemba 7,2023 jijini Dar es Salaam katika mkutano wa jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika(AGRF), Rais Dk.Samia amesisitiza katika zama hizi ICT au teknolojia ya kisasa haiepukiki na inaweza kuingia kwenye sekta ya kilimo

Akifafanua hilo amesema kupitia mitandao na teknolojia ndio wanaweza kuwatoa  fikra vijana kwamba kulima sio kazi ngumu , hivyo teknolojia inakwenda kurahisha kilimo kwa vijana

“Sasa Tanzania tumejua kilimo ni kujua taarifa zake na kwa maana hiyo tunawekeza sana katika tafiti na katika tafiti tunafanya maeneo yote ya kilimo,uvugaji na uvuvi .

“Katika kilimo tumejielekeza sana kwanza kujua afya ya udongo lakini kabla ya kujua afya ya udongo ni kuwa na kanzi data ili kuweza kufanya vizuri.

“Kwa hiyo kwa kutumia ICT tunaendelea kusajili wakulima ,aina ya kilimo wanachofanya, eneo walionalo na mambo mengine yanayomhusu mkulima.”

Ameongeza lakini ili mkulima huyo aweze kufanya vizuri lazima wajue mkulima yuko kwenye hali gani pale alipo, kwa hiyo wamewawezesha maofisa ugani vifaa vya kupima afya ya udongo ,

“Kwa hiyo kila mkulima atakuwa anapimiwa afya ya udongo kutoka muda mmoja kwenda mwingine na kujua kwa uhalisia anatakiwa kutumia mbegu za aina gani…

“Lakini tumejiingiza katika kuongeza uzalishaji wa mbegu za kisasa , tumeimarisha vituo vya utafiti na mashamba ya uzalishaji mbegu kwa kiwango kikubwa ili wazalishe mbegu sana.

“Kwa mfano Arusha kuna kampuni ya mtu binafsi na kuna wengine nao wanazalisha mbegu.Vituo vyetu vya Serikali na vyenyewe tumeviwezesha na tunategemea ikifika 2025 labda robo tatu ya mbegu zitakazotumika kwa zizalishwe hapa nchini kama sio kujitegemea kabisa,”amesema Rais Samia.

Ameongeza na mbezu zinazozalishwa zinatambulika na zinaweza kuhimili mabadiliko  ya hali ya hewa , pia zinaenda na hali ya udongo uliopo.

Rais Samia amesema wanatumia ICT katika masuala ya umwagiliaji kwani kama itakumbukwa zamani wakisema umwagiliaji ilikuwa ni umwagilia haswa kwa maana ya kuchukua maji na kuyamwaga katika udongo ili mazao yaje kama inavyomwaga mvua.

“Sasa tunamwagilia kwa kutumia teknolojia ya kitalaam ambayo mti humwagiliwa kwa maji yanayotakiwa na muda unaotakiwa.Pia tunatumia teknolojia kujua aina ya udongo ulionao unahitaji maji kiasi hiki na sio kiasi hiki na hiyo itasaidia kufanya matumizi mazuri ya maji tuliyonayo.

“Tunakwenda kutumia ICT katika kuhifadhi mazao ya wakulima.Tunajenga  vihenge vya kisasa vinavyotumia mitambo ya kurekebisha mvuke na kuepusha tatizo la kuwa na sumu kuvu katika mazao yetu, tunakwenda kufanya hivyo kwa kutumia ICT,”amesema Rais Samia.

Amesisitiza wanakwenda kutumia ICT kwenye soko kwani lazima wajue taarifa za mahitaji ya matwaka na ugavi wa mazao yanayozalishwa ndani ya nchi.

“Hivyo  ICT haiepukiki , lakini hata teknolojia katika kutayarisha mashamba na tunahitaji kuwa na mitambo ya kisasa na ndio itakayotumika katika mpango wa BBT.”

Amesema ni vizuri kijana akajisikia fahari anapojishughulisha na kilimo na akiendesha trekta liwe la kisasa na linafanya kazi zaidi ya tatu.”Kwa hiyo ICT haiepukuki na Serikali yetu tumedhamiria kuelekea huko.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...