Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika katika Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) leo Septemba 07, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Na Avila Kakingo, Michuzi TV
SERIKALI imesema kuwa sasa ni mapinduzi ya kilimo na wamejipanga katika nyanja mbalimbali li kukifanya kilimo kiwe na tija kwa wakulima na katika jamii.


Ameyasema hayo leo Septemba 07,2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza na vijana waliojiunga na mradi wa Jenga kesho iliyo bora, Building a Better Tomorrow (BBT) katika Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) linaloendelea kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa wamejipanga katika nyanja za Kiteknolojia, Masoko, Usafirishaji, Teknolojia na Tafiti.

Akizungumza akizungumzia kuhusu Tafiti Rais Samia amesema kuwa tafiti mbalimbali zitaendelea kufanyika kuanzia kwenye upimaji udogo ili kujua mbegu gani inaweza kustahimili kwenye udongo gani uliopo kwenye mashamba.

Amesema kuangalia afya ya udongo ni mhimu kwani udongo ukiwa na afya utasaidia katika matumizi ya mbolea

Pia amesema kuwa tafiti zitaboreshwa katika uzalishaji wa mbegu zilizopo hapa nchini ili kufikia mwaka 2025 Tanzania iweze kuzalisha robo tatu (¾) ya mbegu zitakazokuwa zikipatikana nchini ambazo zitakuwa zinastahimili hali ya hewa ya maeneo tofauti tofauti hapa nchini.


TEKNOLOJIA
Rais Samia amesema kuwa teknolojia zaidi inahitajika katika umwagiliaji ili kujua maji kiasi gani yanatakiwa kumwagiliwa katika mashamba na kujua ni muda gani unatakiwa kumwagilia mazao kulingana na maji yaliyopo ili kuepusha kukosekana mwa maji kwa wakati fulani.

Pia amezingumzia kuhusiana na maji ya mvua, amesema kuwa maji ya kumwagilia ni tofauti ya mvua ambayo inakuja kwa bila kipimo. Umwagiliaji amesema utakuja kwa kipimo maalumu ndio maana kuna teknolojia ili wakulima waweze kupima ni maji kiasi gani yanahitajika.

Pia teknolojia itatumika katika kusajili wakulima ili kujua idadi kamili ya wakulima na ni mazao gani wanalima wakiwa maeneo gani.

Kwa upande wa masoko amesema kuwa teknolojia haiepukiki kutakuwa na mitambo ya kisasa ambayo itaweza kutambua ni mazao gani yanhitajika nchi gani au maeneo gani ili kuweza kuendana na mahitaji ya watu.

"Serikali imejipanga kutumia teknolojia ili vijana waondokane na fikra ya kilimo kigumu."

USAFIRISHAJI
Akizungumzia kihusiana na usafirishaji wa mazao Rais Samia amesema kuwa kwa sasa Serikali imeanza kutekeleza mpango wa kutengeneza barabara katika kila wilaya na mikoa ambayo inalima mazao mbalimbali ili kumrahisishia mkulima kuweza kusafirisha mazao kutoka shambani hadi sokoni.

Pia amesema kwa Upande wa Bahari teyari wameanza kujenga gati za kijani katika mikoa ya Tanga, Mtwara, Dar es Salaam na Zanzibar kwaajili ya kusaidia shehena za mazao ili ziweze kusafirisha mazao yanayoharibika haraka ili yaweze kufika salama.

Kwa usafiri wa anga, Rais Samia amesema kuwa tayari shirika la Ndege la Tanzania(ATCL) wameshanunua ndege aina ya Boeing 767-300F kwaajili ya kurahisisha kusafirisha mazao ya kilimo kwenda nje ya nchi.

Pia Rais Samia ametaja viashiria vya jinsi serikali itakavyofanikiwa katika mabadiliko ya kilimo kupitia kwa vijana wa BBT,ambapo BBT itasaidia vijana kutafuta na kushirikiana na watu ambao watakuwa wakiongeza thamani mazao ya vijana.

“Kwa maana vijana wakilima na wakivuna kuwe na mtu anayechukua mazao yote na kuyapeleka kuyaongeza thamani kwenye viwanda vyetu yakiwa yamechakatwa. Kwahiyo hizo ndizo hatua ambazo serikali inazichukua kuimarisha soko.”

amesema kuwa kwa wataangalia maisha ya vijana jnsi yanavyobadilika, matumizi ya mbolea, uzalishaji wenye tija, bei ya chakula kushuka pamoja na mahitaji ya masoko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...