Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
DROO ya tano ya Promosheni ya Maokoto Deilee inayoratibiwa na Sportpesa kushirikiana na Mtandao wa Tigo imefanyika eneo la Tegeta Nyuki, Dar es Salaam huku washindi watatu wakipatikana, wawili wameshinda simu janja (smartphone) na mmoja ameshinda shilingi Milioni moja.

Akizungumza wakati wa droo hiyo, Mwakilishi wa Sportpesa kutoka Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Lydia Solomon amesema washindi wa Simu janja wametoka Dumila, Morogoro na mmoja ametoka mkoa wa Njombe wakati mshindi wa shilingi Milioni moja ametokea mkoa wa Songwe.

“Nawahimiza wateja wetu wa michezo ya kubashiri (Sportpesa) endeleeni kubashiri kupitia Tigopesa kwani zimebaki siku chache mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 15/- atapatikana mwisho wa promosheni hii,” amesema Lydia.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mtandao wa Tigo, Meneja wa Biashara wa Mtandao huo, Kenneth Ndulute amewahimiza wateja wa mtandao huo kuendelea kubashiri michezo mbalimbali kupitia Sportpesa ili kujishindia fedha ambazo zinatolewa na promosheni hiyo ya Maokoto Deilee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...