Rais mstaafu wa awamu ya nne na Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Vyakula Duniani, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika aliyeshika tuzo akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mbegu bora na kilimo katika mkutano wa pembeni wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) linaloendelea kufanyika Septemba 5-8, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
  Rais mstaafu wa awamu ya nne na Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Vyakula Duniani, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa kumtangaza mshindi wa tuzo ya uzalishaji mbegu bora leo Septemba 07, 2023  katika mkutano wa pembeni wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) linaloendelea kufanyika Septemba 5-8, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano wa pembeni wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) linaloendelea kufanyika Septemba 5-8, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu Michuzi Tv
MRADI wa Jenga kesho iliyo bora, (Building a Better Tomorrow (BBT) umetoa fursa kubwa ya ajira kwa vijana na wanawake kuliko sekta nyingine, pia umejenga ushawishi wa vijana wengi kuingia kwenye kilimo.

Hayo ameyasema hayo leo Septemba 7, 2023 na Rais mstaafu wa awamu ya nne na Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Vyakula Duniani, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika mkutano wa pembeni wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) linaloendelea kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Amesema mradi huo ni mhimu hapa nchini kwani umechukua idadi kubwa ya watu.

Katika mkutano huo pia Dkt. Kikwete amemkabidhi tuzo yenye thamani ya million 250 kwa mshindi wa kwanza ambaye alizalisha mbegu bora Afrika.

Tuzo hiyo imenyakuliwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Pan Afrika ya Utafiti wa Maharage, Jean Rubyogo ambaye alifanya kazi ya kuzalisha mbegu bora kwaajili ya kuendleza Kilimo barani Afrika na tuzo hiyo imesimamiwa na Taasisi ya Kimataifa ya Mifumo ya Chakula (AGRA).

Akizungumzia kuhusiana na mashindano ya kuzalisha mbegu bora, Dkt. Kikwete amesema kuwa mashindano yalianza Mei Mwaka huu na mapendekezo yalikuwa 101 na baadae walisogeza muda na yafikia mapendekezo 496, baada ya hapo kamati ikakaa na kuchambua mapendekezo hayo na kufikia 19 na wakaendelea na kuchambua mpaka akapatikana mshindi.

"Wataalamu kutoka AGRA na wengine walichambua mapendekezo haya walipata 19 yakaletwa kwenye kamati yetu kufanya uchambuzi yakabaki mawili tuliunda kamati ndogo kufanya uchambuzi wa hayo mawili hadi kupata mshindi wa leo." Amesema Dkt. Kikwete.

Amesema taasisi iliyochukua tuzo imefanya utafiti wa maendeleo ya mbegu ya maharage aina 650 mbegu zinazo himili changamoto mbalimbali za mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi, kama joto, kuhimili magonjwa na wadudu na maharagwe yake yana madini ya Zinc na chuma.

Aidha amesema mshindi huyo atakabidhiwa tuzo leo jioni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...