Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulua Nchemba akimkabidhi tuzo ya kufanya kazi zaidi ya miaka 20 kama Staff wa kampuni ya Bima ya Alliance, Henry Mgalike wakati wa hafla ya kutimiza miaka 25 kwa  kampuni hiyo. Aliyeko nyuma ya Nchemba ni Kva Krishnan Afisa Mtendaji Mkuu wa Alliance na  aliyeko nyuma ya Mgalike ni Shaffin Jamal  Mwenyekiti wa Alliance.  Hafla hiyo imefanyika Septemba 24,2023 jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya bima ya Alliance KVA Krishna,akizungumza wakati wa hafla ya kutimiza miaka 25 kwa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.


Kamishna wa Bima nchini, Dkt. Baghayo Saqware, akizungumza wakati wa hafla ya kutimiza miaka 25 kwa kampuni ya bima ya Alliance iliyofanyika jijini Dar es Salaam Septemba 14, 2023.
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza wakati wa hafla ya kutimiza miaka 25 kwa kampuni ya bima ya Alliance iliyofanyika jijini Dar es Salaam Septemba 14, 2023.

Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
SERIKALI imesema itaendelea kutengeneza mazingira wezeshi kwa sekta ya bima ili ziweze kukua zaidi na kuchangia katika uchumi.

Amesema watahakikisha wanasimamia sekta hiyo ili ikue zaidi licha ya kukabiliana na changamoto ya uelewa mdogo wa Watanzania kutumia bima.

Akizungumza katika hafla ya miaka 25 ya Kampuni ya Bima ya Alliance, Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema kuwa Kampuni hiyo imefanya kazi kubwa kuhakikisha Watanzania wananufaika na bima kupitia bidhaa mbalimbali.

Amesema Kampuni hiyo imeongezeka bidhaa ya kukabiliana na hali ya hewa zisizotarajiwa kwenye sekta ya kilimo hivyo ni sekta muhimu.

Amesema kuwa miaka 25 ya kutoa huduma za bima, wamewezesha kuvuka mipaka hadi Uganda na kuongeza bidhaa katika sekta ya uzalishaji hususan kilimo.

"Serikali ya awamu ya sita moja ya maeneo ambayo imeweka mkazo ni katika sekta za kilimo, mifugo na Uvuvi na kama Wizara tunaunga mkono kampuni hii kwa kuongeza bidhaa," amesema Dk Nchemba.

Pia Kampuni hiyo itachangia Dola bilioni tano kwa ajili ya kusaidia watoto wa Tanzania hususan watoto wa kike.

"Kampuni hii imepita mikono kadhaa inatoa somo kwa vijana wa Tanzania wanapoanzisha kampuni zao au wanaporithi wasiwaze kugawana bali kuendeleza. Vipo vikundi vinaanzishwa na wanapopata fedha wanagawanyika," amesisitiza.

Dk Nchemba ameeleza kuwa changamoto kubwa inayowakabili sekta hiyo ni elimu ndogo ya umuhimu wa bima na kutokuwepo kwa mtandao mkubwa.

Amesema wataendelea kuwahamasisha Watanzania kutumia bima hizo ili kujikinga yanapotokea madhara mbalimbali.

"Tunaomba Watanzania wachukulie bima ni jambo muhimu kwani hata mataifa mengine duniani yanakuwa kiuchumi kutokana na matumizi ya bima," amefafanua.

Amesema moja ya mabadiliko wanayofanya ni kuruhusu Kampuni binafsi za bima kushiriki katika shughuli mbalimbali ili uchumi uweze kuchangiwa na sekta binafsi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Alliance, Shaffin Jamal amesema kuwa miaka 25 ya kampuni hiyo imeambatana na mafanikio mbalimbali.

Amesema kuwa wamekuwa kufikia mtaji wa Dola bilioni 100 na kuongeza bidhaa mbalimbali katika matawi matano Tanzania.

Jamal amesema Kampuni hiyo imeruhusu imeiruhusu matumizi ya teknolojia na kukuza ustawi wake licha ya kukabiliana na changamoto mbalimbali.

"Kujitolea kwa dhati kwa AICL kumefanya soko la Tanzania kuaminiwa na kwamba uvumbuzi umesababisha kuanzishwa kwa bidhaa na huduma mbalimbali, ikiwa ni pamoja na bima ya kilimo na iliyopachikwa, programu za simu, na huduma za WhatsApp kwa picha," ameeleza Jamal.

Pia amesema kwa kutumia teknolojia ya kidijitali, AICL imeboresha huduma zake, na kuwapa wateja urahisi zaidi, kasi na uwazi katika safari yao ya kutoa bima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...