Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax, Mwenyekiti kikao cha tano cha kamati ya pamoja ya ushirikiano wa katika sekta ya ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 15, 2023 baada ya kufunga kikao cha tano cha kamati ya pamoja ya ushirikiano wa katika sekta ya ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji, katika kikao kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax, Mwenyekiti kikao cha tano cha kamati ya pamoja ya ushirikiano wa katika sekta ya ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 15, 2023 baada ya kufunga kikao cha tano cha kamati ya pamoja ya ushirikiano wa katika sekta ya ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji, katika kikao kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini  na Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, Pascoal Ronda na mkalimani wake.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
SERIKALI Tanzania na Serikali ya Msumbiji zimekubaliana kuendeleza na kudumisha ushirikiano katika Ulinzi na Usalama kwa maslahi kwa Masilahi ya raia wan chi hizo mbili.

Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena  Tax ameyasema hayo leo Septemba 15, 2023 baada ya kufunga kikao cha tano cha kamati ya pamoja ya ushirikiano wa katika sekta ya ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji, katika kikao kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Tanzania iko tayari kufanya kazi kwa karibu na Msumbiji ili kuimarisha zaidi ushirikiano wa ulinzi na usalama.

Amesema kuwa Kwa pamoja, tunaweza kushinda changamoto tunazokabiliana nazo na kujenga mustakabali ulio salama na wenye mafanikio zaidi kwa mataifa hayo mawili kwa watu wake.

Ameeleza kuwa uhusiano wa nchi hizo umejengwa kihistoria tangu wakati wa mapambano ya ukombozi kwa sababu tulipigana pamoja, kushinda pamoja na tunapaswa kubaki na umoja huo.

Akizungumza mara baada ya mkutano uliowakutanisha watendaji wa juu katika Idara mbalimbali za masuala ya ulinzi na usalama kutoka nchi Tanzania na Msumbji Dkt. Tax amesema kuwa mkutano huo ni matunda ya ziara ya Dkt.Rais Samia wa Septemba 27-29, 2022 alipotembelea Msumbiji iliyoendesha majadiliano yaliyowezesha kusainiwa kwa mkataba wa makubaliano ya amani na usalama.

Amesema mkutano huu umetoa fursa nyingine ya kuendeleza kushirikiano hasa katika maeneo ya mashirikiano yaliyomo katika mkataba wa makubaliano.

Kuhusu changamoto za uasi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, Pascoal Ronda amesema uhusiano wa nchi hizo umekuwa na manufaa ya kihistoria.

“Juni 15 mwaka huu ikiwa ni baada ya miaka mingi ya mazungumzo magumu, Rais wa Jamhuri ya Msumbiji pamoja na kiongozi wa chama cha Renamo alifunga kambi ya mwisho ya kijeshi ya vikosi vya kukabili vuguvugu la kigaidi huko Vunduzi, Wilaya ya Gorongosa, Mkoa wa Sofala.”

“Hatua hii ya kihistoria inaashiria mwisho wa mchakato wa upokonyaji silaha, uondoaji na urejeshaji Silaha, uliofanyika kutokana na juhudi za ndani na nje ya Msumbiji na jumuiya ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

“Hatua hiyo inatoa mwelekeo wa maridhiano na utulivu wa nchi huku tukiwa na changamoto kubwa ya kupambana na ugaidi katika Jimbo la Cabo Delgado, ambako ni mapambano ya bila kupumzika huku tukiendelea na ushirikiano wa pamoja na jirani na ndugu zetu Tanzania.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...