Na Karama Kenyunko Michuzi TV
KATIKA kuwahamasisha wafanyabiashara kutumia mashine za kutoa risiti, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imetangaza kuwepo kwa wiki ya mashine za risiti za kielektroniki (EFD) ambayo mbali na mambo mengine,itaambatana na michezo mbali mbali ikiwemo EFD Marathoni.

Katika wiki hiyo ya EFD itakayoanza Septemba 23 hadi 30,202 TRA itajenga mahusiano kati yake na wafanyabiashara na kuhamasisha zaidi matumizi ya mashine za kielektroniki za kutoa risiti.

Akitangaza juu ya wiki hiyo yenye kaulimbiu ya 'Risiti yako, ulinzi wako.' leo Septemba 20,2023 jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema mbali na hayo pia wananchi watakaoshiriki matukio mbali mbali katika wiki hiyo, watapata nafasi ya kuimarisha afya zao kwa kushiriki mchezo wowote kati ya ile ambayo itakuwepo.

"Mpaka sasa maandalizi yote yamekwisha kamilika ambapo zaidi ya watu 2,000 wanatarajiwa kushiriki siku ya ufunguzi kwenye mbio hizo za marathoni za kilomita 5 na 10". Amesema Mpogolo

Amesema, mgeni rasmi katika marathoni hizo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila na kwamba mbio zitaanzia na kuishia viwanja vya Jakaya Kikwete, vilivyopo kidongo chekundu.

Mpogolo amesema mbali na michezo hiyo matukio mengine katika wiki hiyo ni kutolewa kwa elimu ya kodi kwa wananchi na wafanyabiashara katika mikoa ya kikodi ya Ilala na Kariakoo.

Aidha, aliongeza kuwa Septemba 30, 2023 kutakuwa na mechi kati ya maofisa wa TRA wa Ilala na Kariakoo na wafanyabiashara wakubwa na wadogo.

Aidha, Mpogolo amewahimiza wananchi, taasisi na wafanyabiashara kujisajili katika michezo na kupata elimu ya kodi, "Ni wiki ya elimu na kujenga mahusiano baina ya serikali, TRA na wafanyabiashara," amesema Mpogolo.

Mpogolo amezialika klabu za michezo kutoka taasisi na kampuni binafsi kushiriki wiki hiyo akieleza kuwa washindi wote watapata medali na fedha taslimu.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Edward Mpogolo akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) namba na medali zitakazotumika na washiriki wa EFD marathoni katika wiki ya mashine za risiti za kieletroniki (EFD) inayotarajiwa kuanza Septemba 23 hadi 30, 2023 jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja wa TRA mkoa wa kikodi wa Ilala, Masau Malima
Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Edward Mpogolo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake katika kuelekea wiki ya mashine za risiti za kieletroniki (EFD) inayotarajiwa kuanza Septemba 23 hadi 30, 2023.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Edward Mpogolo akionyesha fulana itakayotumika kwenye EFD marathon inayotarajiwa kufanyika Septemba 23, 2023 katika viwanja vya kidongo chekundu jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Meneja wa TRA mkoa wa kikodi Ilala Dar es Salaam Masau Malima na kushoto ni Kabula Mwemezi, Meneja TRA mkoa wa kikodi Kariakoo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Edward Mpogolo akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) namba na medali zitakazotumika na washiriki wa EFD marathoni katika wiki ya mashine za risiti za kieletroniki (EFD) inayotarajiwa kuanza Septemba 23 hadi 30, 2023 jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja wa TRA mkoa wa kikodi wa Ilala, Masau Malima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...