WADAU kutoka Serikalini na mashiriki yasiyo ya Kiserikali wakiwemo wasomi kutoka taasisi za elimu ya juu za ndani na nje mwishoni mwa wiki wamekutana mjini Zanzibar katika semina ya kujadili jinsi ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini ambavyo vimekuwa vikiongezeka mwaka hadi mwaka.

Washiriki wa semina hiyo pia wamepata uzoefu kutoka kwa taasisi zinazoshughulika na wahanga wa changamoto za ukatili wa kijinsia na kubainisha kuwa ili kutokomeza vitendo hivyo kunatakiwa ushirikiano wa pamoja baina ya Serikali ambapo pia walitoa mapendekezo mbalimbali ikiwemo kufanya utafiti wa kina juu ya tatizo na kutafuta ufumbuzi kwa njia ya kisayansi.

Akiongea juu ya tatizo hilo, Mwanzilishi wa taasisi ya Centre to Advance Research on Health in Africa (CAReH Africa), Profesa Gbenga Ogedebde wa Chuo Kikuu cha NYU Grossman nchini Marekani, amesema ni jukumu la wasomi hususani wanasayansi wa kiafrika kufanya tatifi kuhusiana na changamoto zilizopo katika jamii zetu ambazo zitasaidia katika kupata majibu ya kisayansi kuzitokomeza kama lilivyo suala hili la vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Profesa Ogedebde amesema, CAReH Africa, imejipanga kuhakikisha inawezesha kufanyika tafiti za magonjwa barani Afrika sambamba na kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali kupunguza changamoto nyingi za magonjwa na kijamii zilizopo barani Africa ambazo zimekuwa zikipunguza kasi ya kupata maendeleo.

Kwa upande wake, Dkt.Bonus Sizya, kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Care Africa,amesema tatizo la ukatili wa kijinsia kwa sasa limekuwa likigusa makundi yote katika jamii hivyo kunahitajika jitihada kubwa za kuelimisha jamii kupinga vitendo hivi na kuondoa dhana kuwa ni wajibu wa Serikali peke yake kutekeleza jukumu hilo.

Amesema katika warsha hiyo wamejadili mambo mbalimbali yanayopaswa kufanywa na Serikali kama vile masuala ya sera, kuondoa sheria kandamizi, kujenga mazingira rafiki kwa wahanga wakubwa wanaoathirika na vitendo hivi hususani watoto wa kike na kutoa elimu kwa jamii kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ingawa suala hilo pia ni jukumu la wadau mbalimbali ikiwemo kuacha mila potovu ambazo zinachochea kuongezeka kwa vitendo hivi.

Naye, Profesa Chinwe Ogedebde kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Tiba cha Hackenack, amesema ongezeko la vitendo vya ukatili linahusiana pia na changamoto ya ugonjwa wa afya ya akili katika jamii hivyo ni muhimu utafiti kufanyika zaidi na wadau wote kushirikiana katika kulitokomeza.

Watoa mada wote na wachangiaji katika warsha hii walitoa maazimio ya kuendelea kuunnga mkono jitihada za Serikali katika kutoa alimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii sambamba na kushukuru mashirika na taasisi mbalimbali za ndani na nje ambazo tayari zimeanza mapambano ya kukabiliana na changamoto hii.

Afisa Mwandamizi anayeshughulika na masuala ya jinsia kutoka Wizara ya Jinsia,Gift Msowoya, amesema kuwa Serikali tayari imeanza kutekeleza hatua za kupambana ba vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo kutoa elimu kwa jamii na aliwashukuru wadau wote kutoka taasisi zisizo za kiserikali ambao wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa lengo la kutokomeza vitendo hivi.
Mwasisi wa taasisi ya Center to Advance Research on Health in Africa (CAReH Africa), Professor Gbenga Ogedebde ambaye pia ni mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Grossman nchini Marekani akitoa mada wakati wa semina kuhusiana na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini iliyofanyika Zanzibar .
Afisa wa anayeshughulika na masuala ya jinsia, kutoka Wizara ya Maendeleo yaJamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maluum, Gift Msowoya, akitoa mada wakati wa semina kuhusiana na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini iliyofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki
Profesa Manasi Kumar kutoka Chuo  Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, akitoa mada wakati wa semina kuhusiana na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini iliyofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki.


Washiriki wa semina wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa semina hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...