Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje amesema chuo hicho sasa kinajielekeza katika kuachana na matumizi ya makaratasi na kujitika zaidi katika matumizi ya kimifumo katika utoaji wa kozi zake.

Hayo aliyesema Disemba Mosi 2023 wakati wa ufungaji wa kozi mbili ambazo jumla ya Washiriki 31 wamemaliza kozi namba 22 ya Uendeshaji wa shughuli za Usafiri wa Anga (FOO), na wengine 13 katika upande wa kozi namba 20 ya Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga (SMS).

Mkuu wa Chuo kanje alisema kumaliza kwao chuo kuendane na mabadiliko ya tabia na matendo yao, kwani ufaulu wa kwenye cheti pekee hautoshi ila inabidi waonyeshe mabadiliko katika kufanya kazi zao kwa weledi na umahiri mkubwa.

Katika kozi hizo wahitimu wa kozi ya SMS ni watumishi kutoka Shirika la ndege la Tanzania ambao walipata mafunzo ya siku tano na wengine wa FOO walipata mafunzo ya miezi minne.

Mkuu wa chuo Kanje aliongeza kuwa ili kufanikiwa katika masuala ya usafiri wa anga mara nyingi kuna huitaji wa kuwezeshwa na kwa sasa chuo hicho cha CATC kimewezeshwa na kipo kwenye mpango wa kujenga miundombinu yake ya kisasa yenye kuenda na hadhi ya chuo hicho kinachotambulika kitaifa na kimataifa.

Kanje aliwakumbusha washiriki wa kozi hizo mbili kwamba anga ni fedha lakini ili fedha hizo ziweze kupatikana basi ni lazima anga husika liwe salama hivyo ni jukumu la washiriki hao kutekeleza majukumu yao kama maofisa wa FOO na SMS ili kulinga anga.

Kanje aliongeza kuwa chuo cha CATC ni moja ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja kati ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje wakati wa wakati wa ufungaji wa kozi mbili ambazo jumla ya Washiriki 31 wamemaliza kozi namba 22 ya Uendeshaji wa shughuli za Usafiri wa Anga (FOO), na wengine 13 katika upande wa kozi namba 20 ya Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga (SMS)
Mkuu wa Kitengo cha uandaaji mafunzo CATC Thamarat Abeid akitoa ufafanuzi kuhusu kozi kozi mbili ambazo jumla ya Washiriki 31 wamemaliza kozi namba 22 ya Uendeshaji wa shughuli za Usafiri wa Anga (FOO), na wengine 13 katika upande wa kozi namba 20 ya Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga (SMS) wakati wa ufungaji wa kozi hizo.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje(kulia) akiwatunuku vyeti  baadhi ya Washiriki 31 waliomaliza kozi namba 22 ya Uendeshaji wa shughuli za Usafiri wa Anga (FOO)wakati wa kufunga kozi hizo.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje (kulia) akiwakabidhi vyeti wahitimu wa waliomaliza kozi namba 20 ya Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga (SMS) wakati wa kufunga kozi hiyo.
Baadhi ya wahitimu 31 waliomaliza kozi namba 22 ya Uendeshaji wa shughuli za Usafiri wa Anga (FOO), na wengine 13 katika upande wa kozi namba 20 ya Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga (SMS) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje alipokuwa anafunga kozi hizo.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa waliomaliza kozi namba 20 ya Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga (SMS) mara baada ya kufunga kozi hiyo.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu 31 waliomaliza kozi namba 22 ya Uendeshaji wa shughuli za Usafiri wa Anga (FOO) mara baada ya kufunga kozi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...