Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kigawa Mabati kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za jiji la Dar es Salaam ambapo Mabati hayo  yatatumika kama kianzio cha ujenzi wa osteli za wanafunzi wa kike wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kigawa hundi kwa wakuu wa wilaya za jiji la Dar es Salaam ambapo ni fedha zitakazotumika kama kianzio cha ujenzi wa osteli za wanafunzi wa kike wa Mkoa wa Dar es Salaam.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewaomba wadau mbalimbali na wananchi kuwaunga mkono katika Ujenzi wa hosteli kwa watoto wa kike wanaosoma shule za Sekondari za Mkoa huo ili kuwaepusha na changamoto mbalimbali zinazowapata kwani wanawahi kuamka na kuchelewa kufika nyumbani.

Akizungumza leo Januari 19, 2024 wakati wa hafla ya Uzinduzi wa mpango wa Ujenzi wa Hosteli katika Mkoa wa Dar es Salaam 2024 amesema kila halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam inapewa fedha kiasi cha shilingi milioni 20 za kuanzia kujenga huku akiwaasa kuanzisha harambee ya kuchangisha fedha kwaajili ya ujenzi wa hosteli katika halmashauri zao.

Pia amewaomba wanywaji wa bia kumchangia bia moja kwaajili ya ujenzi wa hosteli hizo kwani watakuwa wameokoa wanafunzi wakike ambao ndio wabebaji wa kizazi cha jamii na taifa kwa ujumla.

Chalamila ameendelea kutoa wito kwa mitandao ya simu ambayo itawasaidia kutengeneza namba kwaajili ya wadau mbalimbali kuchangia fedha kwaaajili ya ujenzi wa hosteli hizo.

Maagizo kwa Halmashauri
Mchole ramani za hosteli ambazo mnataka kujenga ambazo zitatakiwa kuchukua wanafunzi kuanzia 80 hadi 120 kulingana na sheria za Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambapo nitakuja kuchagua ramani itakayopendeza.

Chalamila ameeleza kutoridhishwa na kiwango cha ufaulu ndani ya mkoa huo, akisema kuwa muarobaini wa changamoto hiyo ni kuanzisha mpango wa Ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi kwa Shule za Sekondari na Msingi ili kuongeza kiwango cha Ufaulu ambacho kimelegalega kwa miaka ya hivi Karibuni.

"Baada ya Mjadala wetu mkubwa tukaona tumuunge mkono Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwa Januari 27 mwaka huu anaadhimisha Siku yake ya Kuzaliwa, tumeona tumuwahi kwa Kuzindua mpango huu wa Ujenzi wa Hosteli za wanafunzi wa Kike ili kuendana na dhamira yake katika kuimarisha Sekta ya Elimu nchini." Amesema Chalamila.

Aidha Chalamila amesema kundi la Walimu ndani ya mkoa wa Dar es Salaam wanayo nafasi kubwa katika kuhakikisha kiwango cha Elimu na Ufaulu kinaimarika na kutoa matokeo chanya hasa baada ya mpango wa Ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi kukamilika.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amemhakikishia RC Chalamila kuwa Mpango wa ujenzi wa Hosteli kwa mkoa wa Dar es Salaam utakuwa na matokeo Chanya katika kukuza kiwango cha Elimu na Ufaulu wanafunzi kwenye Wilaya hiyo.

Kwa Upande wake Afisa Elimu mkoa wa Dar es Salaam Gift Kyando akitoa Ripoti ya hali ya Elimu na Kiwango cha Ufaulu kwa RC Chalamila amesema kushuka kwa Ufaulu mkoa wa Dar es Salaam, imechangiwa na Kundi la Wanafunzi wanaokwenda Shule asubuhi na Kurejea Nyumbani Jioni.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...