UPANDE wa Jamuhuri katika kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka saba ikiwemo kuisababishia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hasara ya Sh Milioni 954.5.
inayowakabili mafundi wa mashine za kielektroniki za EFD na mwanamke mmoja wamefanyia mabadiliko hati ya mashtaka kwa kumuongeza mfanyabiashara Frank  Kalage

Mshtakiwa Kalage amesomewa mashtaka manne leo Januari 23, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Is-hqa Kuppa na wakili wa serikali Mwandamizi Job Mrema akisaidiana na wakili wa serikali Emmanuel Medalakini pamoja na Auni Chilamula.

Mshtakiwa Kalage ataunganishwa na washtakiwa wenzake Februari 7,2024 ambao ni Awadhi Mhavile, Ally Msesya maarufu kama Ally Yanga (37) mafundi wa mashine za EFD na Salma Ndauka (38) Msimamizi wa Gereji anayeishi Sinza ambapo kwa leo hawakuweza kufika mahakamani kufuatia changamoto za usafiri kutoka gerezani.

Mashtaka dhidi ya Kalage yamesomwa na Wakili Mrema ambapo ameunganishwa kwenye mashtaka ya kutumia isivyohalali mashine za EFD zilizozuiwa na kumpotosha Kamishina, kumdanganya Kamishna wa TRA kwa kutoa risiti zisizo sahihi na kuwanufaisha walipa kodi wengine kudai Sh 954,596,372, kuisababisha TRA hasara na utakatishaji fedha.

 
Wakili Mrema alidai washitakiwa wametenda makosa hayo kati ya Mei na Julai mwaka 2023 ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...