Na Mwandishiwetu, Hanang
TAASISI ya kifedha VisionFund Tanzania kwa kushirikiana na Metro Life Assurance wamewafutia mkopo wadeni ambao ni wafanyabiashara wadogo na wakati 6 ambao ni waathirika wa maporoko ya udongo ya Mlima Hanang mkopo wenye thamani ya zaidi ya milioni 22 huku watano wakisamehewa marejesho ya miezi mitatu kuanzia Januari hadi machi mwaka huu.

Akizungumza leo januari 17 Mkoani Manyara na waathirika hao baada ya kukabidhiwa hundi hiyo ya msamaha kwa wafanyabiashara hao Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja, amesema athari za maporoko hayo yamegusa watu mbalimbali.

Amasema VisionFund Tanzania kwa kushirikiana na Metro Life Assurance waendelee kuboresha ushirikiano na serikali na jamii katika mambo mbalimbali wakati wa shida na raha.

"Jumla ya wafanyabiashara 11 wamapeta athari katika biashara zao ambao 6 wamewafutia mikopo kabisa hawatalipa na watano wamesahemewa marejesho miezi mitatu wataaanza kulipa marejesho rasmii mwezi Apri mwaka huu,"amesema Mayanja.

Amesema kwa kufanya hayo wametambua uhalisia wa taasisi yao kwa kujali wateja wao katika kipindi hiki kigumu kwa kutoa msaada wa haraka na ni muhimu kwa wafanyabiashara hao.

Aidha ametoa rai kwa taasisi zingine za kifedha kuonesha uhalisia na tabia ya taasisi iko je kwa wateja wao wanavyopatwa na magumu na wanawasaidia je katika kipindi hicho.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kifedha VisionFund, Chilala Hakoom amesema lengo kubwa la taasisi hiyo inalenga kusaidia jamii na kuboresha ya mtoto kwa kuwezesha familiakupitia huduma za kifedha.

Amesema taasisi hiyo inatambua ugumu wa kifedha unaotokana na waathirika hivyo imechukua hatua muhimu kufuta mkopo kwa wadeni walioathirika kupitia huduma yao ya Bancassurance.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Metro Life Assurance, Amani Boma amesema wao kama bima wanajukumu la kushiriki katika jambo hilo kwa sababu wanahusika na majanga.

"Ni wajibu wetu kuungana na kushirikiana serikali katika masuala ya majanga na bima kushiriki kwa wakati na watanzania mnapaswa kuwa na bima ziwasaidiea wakati wa matatizo,"amesema Boma.

Kwa upande Mfanyabiashara wa Katesh, Fura Massawe ambaye ni muathirika wa maporoko hayo amesema anawashukuru VisionFund kwa kutambua changamoto zinazowakabili kwa sasa ikiwemo kupoteza mali zilisombwa na maji hivyoo wanaanza upya biashara.

Maporomoko ya udongo na mawe kutoka eneo la mlima Hanang yaliyokea Desemba 3 mwaka 2023 na kusababisha vifo vya watu 89 na kuacha zaidi ya 600 bila makazi hususan kwenye kata za Gendabih,Ganana na Katesh



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...