Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Zanzibar, wamefurahishwa na elimu ya hali ya hewa inayotolewa katika maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, yanayofanyika katika viwanja vya Maonesho ya Biashara, Nyamanzi, Mjini Magharibi, Zanzibar kuanzia Tarehe 07 – 19 Januari, 2024.

Wageni mbalimbali waliweza kutembelea banda la TMA wakiwemo viongozi wa Taasis kutoka Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Prof. Ulingeta Mbamba, Shirika la Reli Tanzania Bw. Masanja Kadogosa, Mkurugenzi wa Huduma za Taasis kutoka Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Hamidu Mbegu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Bw. Teophoy Mbilinyi ambao waliipongeza TMA kwa huduma nzuri ya usahihi wa Utabiri inayotolewa .

Aidha, wataalam wa hali ya hewa kutoka TMA wameendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ili kutumia huduma mahususi zinazotolewa na TMA pamoja na kuelewa namna ya kutumia taarifa za hali ya hewa kwa usahihi ili kukabiliana na athari zitokanazo na hali mbaya ya hewaMichuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...