WATANZANIA wamehimizwa kujikita katika matumizi ya simu janja ili kutafuta fursa za kibiashara hatua ambayo itasaidia kuondokana na ombwe la utegemezi kwa serikali pamoja na jamii inayowazunguka.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Mkuu wa kitengo cha biashara ya simu za mkononi ya Samsung Tanzania, Mgope Kiwanga wakati wa uzinduzi wa simu mpya lengo ni kuleta uchechemuzi wa kibiashara.

Amesema pamoja na mambo mengine Samsung Tanzania imetenga fedha ili kuwawezesha wafanyabiashara mtandao kwa kutumia simu janja ili kuongeza ufanisi wa biashara kwa wafanyabiashara wadogo na wakati –SME’s.

‘’Kitu ambacho kinatutofautisha sisi na wengine wote Samsung tunatoa simu za mkopo kupitia washirika wetu kama vile kampuni za mawasiliano ikiwemo Tigo na Vodacom kwahiyo wananchotakiwa ni kuwa waaminifu’’ Alisema Kiwanga.

Aidha amesema simu hizo ni Galaxy S24 Ultra, Galaxy S24 ambapo amesema hatua ya kuzinduliwa simu hizo kwa pamoja Duniani kote ni urithi wa uvumbuzi.

Kampuni ya Samsung imesema zoezi la kuanza kuagiza simu hizo mpya kwa upande wa Tanzania litaanza Januari 18 hadi Februari 13 mwaka huu pamoja na kutoa zawadi mbalimbali.

Imeelezwa kuwa simu janja za Galaxy S24 pamoja na nyingine zilizozinduliwa zimetajwa kuchochea ubunifu wa matumizi ya vifaa vya kidigitali vinavyotumia teknolojia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...