Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa imezindua promosheni ya Swahiba "Langu Lako" inayolenga kuwahamasisha wananchi na wateja wa benki hiyo kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo SimBanking, Lipa Hapa na Hodari Account ambayo ni maalum kwa ajili ya wafanyabiashara.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika Jumanne Februari 13, 2024 jijini Mwanza, Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta amewamasisha wananchi kutumia huduma za benki hiyo ikiwemo Lipa Namba kwa ajili ya kulipia bidhaa malimbali badala ya kutembea na fedha taslimu.

"Tumekuja na akaunti ya Fahari Account kwa ajili ya wafanyabiashara ambapo inawawezesha kuweka na kutoa pesa bila makato huku ikiunganishwa na huduma ya Lipa Hapa ambapo wateja watalipia bidhaa. Pia ukifungua akaunti hiyo, unaweza kupata huduma za mikopo hivyo wafanyabiashara nawasihi kuchangamkia Hodari Account" amesema Sitta na kuongeza;

"Swahiba ni wewe rafiki yangu, ni wewe mteja wa benki ya CRDB hiyo tunataka kila mfanyabiashara ambaye ni Swahiba wa CRDB kufungua Hodari Account ili kunufaika na huduma ya lipa namba, kuweka na kutoa fedha bila makato pamoja na kupata mikopo hadi milioni 50" amesema Sitta.

Meneja Mwandamizi wa CRDB Huduma Mbadala (SimBanking), Mangire Kibanda amesema wateja wanaoendelea kutumia huduma za benki hiyo ikiwemo SimBanking wanayo fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo gari, runinga, simu janja pamoja na kompyuta mpakato, ikiwa ni maana halisi ya wateja kuwa Swahiba na benko hiyo.

"Tunaposema Swahiba, Langu Lako tunamaanisha shida za mteja ni shida za benki ya CRDB ambayo ina mazingira sahihi ya kupata usuluhishi wa shida hizo" amesema Meneja wa CRDB Tawi la Mwanza, Medard Kayombo akisisitiza umuhimu wa kutumia huduma za benki hiyo.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta akizungumza kwenye uzinduzi wa promosheni ya Swahiba, Langu Lako inayolenga kuhamasisha huduma za benki hiyo ikiwemo Lipa Hapa, Hodari Account na SimBanking.
Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta akizungumza kwenye uzinduzi wa promosheni ya Swahiba, Langu Lako inayolenga kuhamasisha huduma za benki hiyo ikiwemo Lipa Hapa, Hodari Account na SimBanking.
Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Medard Kayombo akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Swahiba, Langu Lako.
Meneja Mwandamizi wa CRDB Huduma Mbadala (SimBanking), Mangire Kibanda akieleza namna wateja wa benki hiyo wanaweza kujishindia zawadi mbalimbali kwa kutumia huduma zake ikiwemo SimBanking.
Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta (kushoto) akimkabidhi zawadi ya runinga Jackson Kapele (kulia) ambaye ni mtoa huduma aliyesajili wateja wengi wa SimBanking kwa mwaka 2023 jijini Mwanza.
Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta (kushoto) akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Jackson Kapele (kulia) ambaye ni mtoa huduma aliyesajili wateja wengi wa SimBanking kwa mwaka 2023 jijini Mwanza. 
Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta akiwa kwenye picha ya pamoja na watoa huduma wa benki hiyo baada ya uzinduzi wa promosheni ya Swahiba, Langu Lako inayolenga kuhamasisha wananchi na wateja wa benki ya CRDB kutumia huduma za benki hiyo.
Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta akiwa kwenye picha ya pamoja na watoa huduma wa benki hiyo baada ya uzinduzi wa promosheni ya Swahiba, Langu Lako inayolenga kuhamasisha wananchi na wateja wa benki ya CRDB kutumia huduma za benki hiyo.
Benki ya CRDB imejipanga kuwafikia wafanyabiashara jijini Mwanza ili kuwasajili na Hodari Account itakayowawezesha kupokea malipo ya bidhaa wanazouza kupitia Lipa Namba/ Lipa Hapa, kuweka na kutoa fedha bila makato pamoja na kunufaika na mikopo mbalimbali hadi shilingi milioni 50 ili kukuza zaidi biashara zao ambapo promosheni hiyo ilianza mwezi Januari 2024 huku ikizinduliwa rasmi Februari 13, 2023 Kanda ya Ziwa.
SOMA ZAIDI>>> HABARI ZAIDI HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...