WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michez, Dk Damas Ndumbaro anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio za mwaka huu za Kilimanjaro International Marathon zinazotarajiwakufanyika Moshi, mkoani Kilimanjaro, Februari 25.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wandaaji wa mashindano hayo, tayari Waziri Ndumbaro amethibitisha kushiriki hafla hiyo ambapo anatarajiwa kuongozana na viongozi wengine wa ngazi ya Mkoa wa Kilimanjaro na wa ngazi ya Kitaifa katika shughuli hiyo.

"Wakati wa hafla hiyo, Waziri Ndumbaro anatarajiwa kuanzisha rasmi mbio za kilomita 42 na zile za kilomita 21 na kasha yeye mwenyewe kushiriki mbio za kilomita 5 za Gee Soseji”, ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa matayarisho yoteyamekamilika na kwamba maonyesho maalaum yajakulikanayo kama Kili Expo yanayotangulia tukio la marathon na ambayo yanafanyika kwa msimu wa tatu sasa yanatarjiwa kuanza Alhamisi Februari 22, katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).

Taarifa hiyo imeeleza kuwa katika maonyesho hayo wadhamini mbalimbali wa mbio hizo za kimataifa wanatarajiwa kuonyesha bidhaa, huduma na shughuli mbalimbali wanazozifanya kupitia taasisi zao.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa maonyesho hayo ya siku nne yanaenda sambamba na ukusanyaji wa namba na vifaa kwa ajili ya washiriki wa mbio za Kili Marathon katika viwanja vya MoCU, kuanzia siku ya Alhamisi Febuari 22, saa 6 mchana hadi saa 11 jioni, Ijumaa Februari 23, kuaniza saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni na Februari 24, kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni.

Waandaaji wametoa wito kwa wanaotarajia kushiriki mbio hizo kuzingatia muda na siku zilizowekwa kwa ajili ya uchukuaji namba, ambapo wale watakaokwenda kuchukua namba na vifaa kwa niaba ya washiriki halisi watatakiwa kuwa na nyraka za uthibitisho kutoka kwa washiriki halisi waliowaagiza ili kuepuka usumbufu.

"Ni matumaini yetu kwamba washiriki watajitokeza kwa wingi ili kuchukua namba na vifaa vyao vya ushiriki kama ilivyoelekezwa maana namba au vifaa havitatolewa siku ya tukio hata kwa wale waliojiandikisha kwa kufuata taratibu zote”, ilisema taarifa hiyo.

Aidhaa taarifa hiyo imetoa onyo kali kwa wale wanaotarajia kushiriki kwa kutumia namba ambazo hazikutolewa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa, ambapo wandaaji wamesema watakaobainika wataondolewa kwenye mashindano hayo na kwamba hao ni pamoja na wale watakaobanika kutumia namba za watu wengine sambamba na wale watakaotumia namba za miaka ya nyuma. kutoka kwa mbio.

"Kamati ya wandaaji pia inatoa onyo kwa wale wanaoendesha zoezi haramu za kuuza tiketi za bandia kwenye mitandao, hawa wanafuatiliwa kwa makini na watakapobainika, hatua kazi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao”, ilisema taarifa hiyo.

Wadhamini wa mwaka huu ni pamoja na wadhamini wakuu Kilimanjaro Premium Lager, Tigo -21km Half Marathon, Gee Soseji – 5 km Fun Run, wadhamini wa meza za maji- Kilimanjaro Water, TotalEnergies, CRDB Bank, Simba Cement na TPC Sugar. Wabia wakuu – Garda World, CMC Automobiles, Salinero Hotel na wasambazaji – Kibo Palace Hotel na Keys Hotel.

Kili Marathon huandaliwa na Kilimanjaro Marathon Company Limited na kuratibiwa kitaifa na Executive Solutions Limited.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...