Waandaaji wa Kilimanjaro Premium Lager International Marathon wametangaza utaratibu wa uchukuaji namba na vesti za kukimbilia kwa waliojisajili.

Hatua hii inakuja baada ya usajili wa mbio hizo kwani nafasi zilishajaa kwa mbio za KM 42 na 21 kabla ya Februari 6, 2023 ambayo ilikuwa tarehe ya mwisho ya kujisajili.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na waandaaji wa mbio hizo ilisema bado kuna nafasi kwa mbio za Gee Soseji KM 5 Fun Run. Washiriki wanaweza kujisajili kwa kupitia Tigopesa kwa kupiga *150*01#, kasha kubonyeza 5 LKS, kisha 5 (Ticket) na kufuata maelezo ili kukamilisha usajili au kwa njia ya mtandao kupitia www.kilimanjaromarathon.com.

Taarifa ya waandaaji hao ilisema kuwa zoezi hilo litaanzia Jijini Dar es Salaam Jumamosi Februari 17 na 18 mwaka huu katika viwanja vya Mlimani City kuanzia saa sita mchana hadi saa kumi na mbili jioni.

Baada ya Dar es Salaam, zoezi hilo litahamia Arusha katika hoteli ya Kibo Palace Februari 20 na 21 kuanzia saa nane mchana hadi saa moja jioni.

Kituo cha mwisho ni Moshi Mjini ambapo zoezi hilo litafanyika Februari 22 (saa sita mchana hadi saa kumi na moja jioni), Februari 23 (kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni) na Februari 24 (kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni) katika uwanja wa Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (MoCU).

Waandaaji hao wametoa wito kwa washiriki kuzingatia muda katika kila kituo ili kuepusha usumbufu na pia walitoa wito kwa wanaowachukulia washiriki wengine namba zao wahakikishe wanaenda na nakala ya kitambulisho au barua kutoka kwa mshiriki halisi.

“Ni matumaini yetu kuwa washiriki watajitokeza kwa wingi Jijini Dar es Salaam na Arusha ili kupunguza msongamano Mjini Moshi,” ilisema sehemu ya taarifa ya waandaaji hao.

Waandaaji hao pia wamesisitiza kuhusu hatua zitakazochukuliwa dhidi ya watu wanaodaiwa kuuza tiketi mtandaoni kwa njia isiyo halali. “Wau hawa watachukuliwa hatua za kisheria kwa sababu ni marufuku kuuza tiketi bila idhini ya waandaaji na hata hivyo usajili umeshafungwa,” ilisema taarifa hiyo.

Watakaokimbia na namba feki zikiwemo za miaka iliyopita pia watachukuliwa hatua ikiwemo kuondolewa mashindanoni, kufutiwa matokeo na pia kufungiwa kushiriki katika Kilimanjaro Marathon kabisa.

Wadhamini wa mbio za mwaka huu ni Kilimanjaro Premium Lager-42km (mdhamini mkuu), Tigo- 21km Half Marathon, Gee Soseji – 5Km Fun Run, wadhamini wa meza za maji Simba Cement, Kilimanjaro Water, TotalEnergies, CRDB Bank and TPC Sugar, wabia rasmi-Garda World Security, CMC Automobiles, Salinero Hotels and na wasambazaji rasmi - Kibo Palace Hotel and Keys Hotel.

Mbio za Kilimanjaro International Marathon, zinazotarajiwa kufanyika Jumapili Februari 25 mwaka huu huandaliwa na Kilimanjaro Marathon Company Limited na kuratibiwa kitaifa na Executive Solutions Limited.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...