Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela, Mkurugenzi Mtendaji wa Dough Works, Vikram Desai,  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oryx Energies Tanzania, Kalpesh Mehta wakishirikiana na wafanyakazi wa tawi jipya la jijini Arusha leo Februari 13, 2024 wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mgahawa wa KFC jijini humo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela akizungumza leo Februari 13, 2024 wakati wa uzinduzi wa Mgahawa wa KFC jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Dough Works, Vikram Desai akizungumza leo Februari 13, 2024 wakati hafla ya uzinduzi wa Mgahawa wa KFC jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oryx Energies Tanzania, Kalpesh Mehta akizungumza leo Februari 13, 2024 wakati hafla ya uzinduzi wa Mgahawa wa KFC jijini Arusha.

KATIKA kuhakikisha watanzania pamoja na wageni wanaofika nchini kutalii wanapata huduma bora ya chakula, Mgahawa wa KFC umefungua tawi Jijini Arusha leo Februari 13, 2024.

Tawi hilo linakuwa la tisa kufunguliwa hapa nchini tangu mgahawa huo wa kimataifa wenye Makao yake makuu nchini Marekani kufungua tawi lake la kwanza Jijini Dar es Salaam mwaka 2013.

Mkurugenzi Mtendaji wa Dough Works, Vikram Desai akizungumzia kuhusiana na uamuzi wa kufungua  KFC Jijini Arusha amebainisha kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa Tanzania kwa kuwa mbali na kuwafikishia wananchi huduma bora ya chakula lakini pia inachangia ajira kwa watanzania.

Amesema, Arusha ni Jiji la kitalii ambapo watalii wamekuwa wakifika kwa wingi kutalii, hivyo kwa uwepo wa KFC itawapatia huduma za chakula chenye hadhi ya kimataifa.

"Leo ni siku nzuri kwetu kampuni ya Dough Works kwa kuwa tunaungana na serikali katika kuimarisha huduma kwa watalii, huu mgahawa wa KFC ni wa kimataifa na upo kwenye nchi zaidi ya 140 hivyo watalii wakifika Arusha na kukuta kuna KFC kama kati ya huduma za chakula wanafurahi zaidi.” Amesema

Amesema kuwa baada ya kufungua tawi la Arusha itafuata zamu ya Dodoma na Zanzibar.

“Tunashukuru kufika Arusha lakini naomba muongeze zaidi migahawa yenu maana Arusha ni jiji la kitalii lakini pia nashukuru ajira kwa vijana vinakua kutokana na bidhaa mzazouza ikiwemo serikali kupata mapato.” Amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oryx Energies Tanzania, Kalpesh Mehta amesema kuwa kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha inashirikiana na kampuni ya Dough Works Tanzania katika kuhakikisha huduma ya KFC inatolewa kwa ufanisi hapa Arusha.

Kwa Upande wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela ameshukuru kwa kufunguliwa kwa mgoahawa huo Mkoani Arusha pia ameuomba Mkurugenzi Mtendaji wa Dough Works, Vikram Desai kufungua Migahawa hiyo mingi zaidi ili vijana waweze kupata ajira katika jijini hilo la kitalii.

“Tunashukuru kufika Arusha lakini naomba muongeze zaidi migahawa yenu maana Arusha ni jiji la kitalii lakini pia nashukuru ajira kwa vijana vinakua kutokana na bidhaa mzazouza ikiwemo serikali kupata mapato.” Amesema

“Kwa kuwa hapa ORYX kuna huduma mbalimbali mbadala zinazoendana na huduma za magari ikiwemo service za magari au uoshaji wake pamoja na huduma nyinginem kwetu kufanya kazi na Dough Works katika biashara ya KFC tutawafikia wateja wengi zaidi.” Amesema Mehta

Migahawa ya KFC hapa nchini inapatikana Mlimani City Mall, Masaki, Diamond Plaza-City Center, Mikocheni Plaza, Kariakoo, Morocco, Mbezi Beach na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...