Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemuachia huru Miriam Mrita, ambaye ni mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara wa madini mkoani Arusha, Erasto Msuya, maarufu kama Bilionea Msuya na mwenzake Rovocatus Muyella (Ray) kufuatia ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.
Miriam na Ray ambao wamekaa rumande kwa zaidi ya miaka saba wameachiwa huru leo Februari 23, 2024 majira ya saa moja usiku na Jaji Edwin Kakolaki baada ya kumaliza kusomwa kwa hukumu yao iliyoanza mapema saa 5:01 asubuhi na kumalizika saa 1:07 usiku.
Mara baada ya kusomwa kwa hukumu huyo vilio vya furaha kutoka kwa ndugu wa washtakiwa na vilio vya simazi kutoka kwa ndugu marehemu vilisikika kwa wakati mmoja baada ya ukimya wa muda mrefu kutawala muda wote wa kusomwa kwa hukumu hiyo katika chumba cha wazi namba moja cha mahakama hiyo.
Agosti 23,2016 Miriam alifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Agosti 23,2016 akituhumiwa kumuua wifi yake, Aneth Elisaria Msuya aliyeuawa Mei 26, 2016 kwa kuchinjwa nyumbani kwake Kibada, Kigamboni, wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam.
"Mahakama imejiridhisha kwamba upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa, mahakama inawaona hawana hatia na hivyo inawaachia huru kwa kosa linalowakabili na nina elekeza huko gerezani wawaachie labda kama wanamakosa mengine,"amesema Jaji Kakolaki
Mara baada ya Jaji Kakolaki kutamka "baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili, mahakama imeridhika kwamba upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa bila kuacha shaka yotote...., ghafla hali ya ukimya iliyokuwa imetawala ilipotea na sauti ilisikika ikisema "Yesu umetenda na damu ya mtu iliyomwagika italipwa na kelele mbali hali iliyomfanua jaji Kakolaki kunyamaza kwa muda kuendelea kusoma hukumu.
Mjane wa bilionea Msuya nae akiwa ndani ya kizimba alilala chini huku akilia kwa uchungu akimshukuru Mungu kwa kuachiwa huru ndipo askari Magereza akamuinua ili kuweka utulivu jaji aendelee.
Lakini ghafla ndugu mmoja wa marehemu Aneth ambaye hakufahamika jina alipiga kelele akiwa kwenye benchi la mahakama na kisha akaanguka chini akilia kwa uchungu huku akisema "damu ya Aneth watailipa wote waliohusika akaanza kugala gala chini huku jaji akiwa bado hajatoka nje ya chumba cha mahakama na bado alikuwa hajamaliza kusoma hukumu.
Askari wa kike alimfuata dada huyo na kumwambia kwamba mahakama inaendelea anatakiwa aache kelele na aende nje, akaanza kuzungumza kwa sauti kubwa huku akilia kwa uchungu kwamba haogopi kufungwa kwa sababu ndugu zake wameshauwawa.
Aliendelea kupiga kelele akidai kuwa wamfunge tu haogopi kitu chochote, wakati ndugu wa Mrita ambao wao walikaa upande wa kulia wa chumba hicho walinyamanza kimya kusikiliza kinachofuata wakati ndugu wengine wa marehemu Aneth wakiwa wamejitenga.
Baada ya hayo, Jaji Kakolaki alimalizia kusoma hukumu hiyo akiamuru gari aina ya Rangerover ambalo lilitolewa mahakamani hapo kama kielelezo litaifishwe na kuwa mali ya serikali kwa sababu halina mtu kwani hata katika mirathi gari hilo halipo.
Awali akitoa sababu za kuwaachia huru washtakiwa hao, jaji Kakolaki amesema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kama mjane huyo alikuwepo eneo la tukio na kwamba hakuna muunganiko wowote wa ushahidi unaomtia hatiani.
"Ili Mrita aweze kuunganishwa katika mauji hayo, upande wa mashtaka ulitakiwa kuchukua sampuli ya ya vielelezo vilivyokuwepo katika tukio ili viweze kuunganishwa na sampuli za mshitakiwa kwa sababu vinasaba vinaeleza kwamba damu iliyokuwepo kwenye kisu ni ya jinsia ya kike,lakini hakusemwa ni ya nani,"amesema
Pia, alisema mahakama imebaki na mashaka kama kisu kilichotumika kumchinja Aneth ndicho kilichokutwa eneo la tukio kutokana na kwamba vinasaba vinaonesha kwamba vinasaba vya mshtakiwa Muyela vinafanana na vinasaba vya kwenye kisu na filimbi, kwa hiyo inawezekana yeye ndiyo aliyefikisha eneo la tukio au kuvitumia.
Jumla ya mashahidi 25 wa upande wa mashtaka, mashidi watano wa utetezi na vielelezo 31 viliwasilishwa mahakamani hapo wakati wa uskilizwaji wa kesi.
Upande wa mashtaka katika kesi hiyo uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Paul Kimweri, Yasinta Peter , Marietha Maguta na Generosa Montano huku utetezi ukiongozwa na wakili Peter Kibatala aliyekuwa akkimtetea mjane Miriam na Nehemia Nkoko aliyekuwa akimtetea Muyella

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...