Baadhi ya watalii wakishuka uwanja wa ndege wa Hifadhi ya Saadani
*Yaahidi wataofika watafurahi na kuandika historia mpya.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
HIFADHI ya Saadani imesema kuwa katika kusherekea Sikukuu ya Wapenda nao ambayo hufanyika kila Mwaka Februari 14 'Valentine Day' Hifadhi hiyo imejiandaa kupokea wageni wengi.
Wataofika kwenye sherehe wataandika historia mpya kutokana vivutio vilivyo katika hifadhi ya Saadani.
Baadhi vivutio ni vya ufukwe wa Bahari,kutalii kwa boti kuangalia wanyama kiboko ,Mamba ,Maji ya Mto wa Wami yanavyoingia Bahari pamoja na wanyama.
Hayo ameyasema Afisa Uhifadhi Mwandamizi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani Prisca Eliasi wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo.
Amesema kuwa gharama zake katika kusherekea ni ndogo nia ni kufanya kila Mtanzania kufurahia mazingira mazuri.
Amesema mikakati wageni wote wataofika katika kusherekea watapata malazi katika mazingira ya utouti na walikotoka na utulivu wa aina yake.
Amesema kuwa Valentine Day itakuwa na utofauti kwa kuwa na wasanii wataotumbwiza katika viwanja vya hifadhi hiyo.
Amesema wananchi Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani pamoja na Tanga kwenda kupata mandhari tofauti ya siku ya wapenda nao ili wajionee Vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo.
Amesema.
Hifadhi ya Saadani imezidi kupokea watalii kutoka mataifa mbalimbali kutokana na upekee Utalii kwa Afrika Mashariki wa Hifadhi hiyo kutoka Nyikani kuingia Baharini.
Amesema asilimia 70 katika hifadhii ya Sadani ni eneo la nchikavu na asilimia 30 ikiwa ni eneo la Bahari ya Hindi huku kukiwa na uwepo wa Vivutio tofauti tofauti vya kitalii katika hifadhi ya saadani ikiwemo Kasa wa Kijani.
Amesema Hifadhi ya Saadani imekuwa ikishangaza watalii Watalii kutokana na aina mbalimbali za Viumbe hai vilivyopo.
Prisca amesema uwepo wa Viumbe maji ikiwemo kamba mti na miamba ya kipekee ya mazalia ya samaki katika kisiwa cha Mafui San Bank kinachopatikana katikati ya bahari ya Hindi kumeendelea kuwavutia watalii na kuendelea kuwa umaarufu wa kipekee duniani.
Aidha amesema katika hifadhi ya saadani miongoni wa Vivutio vya kipekee ni uwepo wa kisiwa cha Mafui San Benk ambacho Watalii wengi ufika na kwenda kukiangalia ambapo maji yake ufika nchikavu nakuacha mchanga unaovutia katika kisiwa hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...