WADAU wa Maendeleo kwa kushirikiana na Serikali wameitaka jamii kuendelea kukemea vikali vitendo vya ukatili vinavyofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waadilifu jambo ambalo linapelekea kuongezeka kwa mmong'onyoko wa maadili  na kuacha baadhi ya familia kukosa malezi na kuwa na hali ya tegemezi Nchini.

Akizungumza leo Machi 13, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati Wadau wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia kutoka nchini Ethiopia walipotembelea Kituo Cha Taarifa na Maarifa Kata ya Majohe kwa lengo la kujifunza na kubadilishana changamoto za ukatili, Mwanachama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Rehema Mwateba, amesema kuwa wakati umefika wa kuzungumza ukweli kuhusu Ukatili unaofanyika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo Cha Taarifa na Maarifa Kata ya Majohe Tabu Ally, amesisitiza umuhimu wa kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wa matukio hayo na akienda mbali zaidi kuiomba serikali kuweka sheria kali juu ya watu ambao wameendelea kufanya vitendo visivyo rafiki katika jamii husika.

Aidha, aliongeza kuwa kuna hitajika jitihada za wadau mbalimbali wa maendeleo na serikali kutoa elimu kwa baadhi ya watu ambao bado wanauelewa mdogo kwenye masuala ya haki ya binadamu ili kupunguza vitendo vya ukatili, pia amewataka watumishi wa umma wakiwemo Mawaziri, Wabunge na viongozi wengine wa ngazi za juu kutembea kwenye majimbo hasa ya ngazi za nchini ili kujionea vitendo vya kikatili vinavyozidi kushamiri hasa kwa watoto wa kike wenye umri mdogo.

Naye Mkazi wa Mtaa wa Kivule Majohe Wivina Alkadi, ambaye alifanyiwa ukatili na Mume wake kwa kuwabaka wanaye wawili na mmoja kumpa ujauzito jambo ambalo lilipelekea mtuhumiwa huyo kufungwa kifungo cha miaka 60 jela ambapo ameiomba jamii iweze kumsaidia baadhi ya mahitaji ya Familia kwani anaishi katika mazingira magumu.

Pia ametumia fursa hiyo kuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na watanzania kiujumla kumsaidia ili watoto wake waweze kuendelea na masomo kwani wananishindwa kusoma kutokana na hali ya maisha ambayo amekuwa akiyapitia mama huyo mara baada tu ya mume wake kuhukumiwa kifungo cha miaka 60 jela.

Huku Wadau wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia kutoka nchini Ethiopia Rediet Asfew wamesema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwa TNGP katika kufanya uwezeshaji wa kiuchumi kwa Wanawake ili kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na wadau na serikali katika kuhakikisha masuala ya ukatili yanadhibitiwa ili kumkwamua mwanamke kiuchumi .
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...