JUKWAA la viongozi wanawake wa Mashirika ya umma limetoa tuzo maalumu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kama ishara ya kumuunga mkono na kumpogeza jwa kazi ambazo amekuwa akiizifanya.

Akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Dkt Samia Suluhu Waziri wa maendeleo ya jamii Jinsia, wanawake na Makundi maalumu Dkt Dorothy Gwajima katika hafla iliyowakutanisha wanawake hao katika kusherekekea siku ya wanawake duniani ambayo uadhimishwa kila ifikapo Machi 8.

Amesema atahakikisha anafikisha salamu kuwa wanawake hao wanasimama na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika ajenda zake sambamba na kumuunga mkono uongozi anaoutoa katika nchi.

Dkt Gwajima amesema kupitia dhana ya usawa wa kijinsia katika sekta zote ikiwemo ya uongozi itasaidia kuwainua wanawake waliokata tamaa kuzingumza kwa vitendo na kusimamia imara.

” Tutakaposimamisha uongozi katika ngazi zote tutaweza kunusuru mambo ambayo yamekuwa chagamoto katika jamii kwani wanawake ni zaidi ya asilimia 51 huku duniani ni nusu”amesema Dkt Gwajima

Alisisitiza kuwa kusimama kwa wanawake katika nafasi mbalimbali aimaanishi kushindana na wanaume bali ni kila mmoja kutimiza majukumu yake yanayomuhusu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya biashara Tanzania (Tantrade) Latifa Mohamed Hamis amesema wameamua kuungana pamoja kwa lengo la kubadilishana uzoefu, na kuutumia kwa ajili ya kujipanga na kutathimini masuala mbalimbali .

“Siku hii muhimu kwetu sisi kama wanawake viongozi wa Taasisi za umma kuwa sehemu ya sherehe zetu kukutana na kujitathimini pamoja na kubadilishana mawazo yetu yatayoweza kusaidia jamii zetu tunazoziogoza”amesema Latifa

Amesema kwa mara ya kwanza wanawake viongozi wa Taasisi za umma wameamua kukusanyika pamoja, na kueleza kuwa mikutano hiyo itakuwa endelevu ili kuhakikisha majumuiko hayo yanaleta faida katika jamii wanazoziogoza.

Aidha amesema ipo haya ya jukwaa hilo kuwashirikisha wanawake wengine katika ngazi za Kata, mikoa wilaya ili waweze kuwafaidisha pia.

“Siku hii muhimu kwetu sisi kama wanawake viongozi wa Taasisi za umma kuwa sehemu ya sherehe zetu kukutana na kujitathimini pamoja na kubadilishana mawazo yetu yatayoweza kusaidia jamii zetu tunazoziogoza”amesema Latifa

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa usimamizi wa hakimiliki kutoka Ofisi ya hakimiliki Tanzania (COSOTA) Doreen Sinare amesema umoja huo upo katika malengo tofauti ikiwemo ya kujisajili ili kuhakikisha unatimiza malengo ambayo umejiwekea.

Sinare amesema Umoja huo unaundwa na kamati ya mpito ambayo inahususisha viongozi wa Taasisi za umma.

Aidha amesema mbali na kutoa tuzo jwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia wametoa tuzo.

Kwa wakuu wa Taasisi wanamke katika nafasi zao kutokana na kufanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanatimiza malengo ya kitaasisi na yaliyowekwa na nchi.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...