Meneja Rasilimali watu wa ALAF Limited Jumbe Onjero, akizungumza katika maonyesho ya kazi kwa wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) wakati yaliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) wakifuatilia Kwa makini wakati wa hafla hiyo.











Mkurugenzi wa Taaluma wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Dk. Kilaza Mwaikono akizungumza katika maonyesho hayo ya kazi. 
Mkuu wa Kitengo cha mabati ya rangi wa kiwanda cha ALAF Limited, Mhandisi Tumani Minja, ambaye pia ni mwanafunzi  wa zamani wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) akizungumza katika maonyesho ya kazi DIT. Hafla hiyo iliyoratibiwa na ALAF Kwa kushirikiana na DIT, ilifanyika mwishoni mwa wiki Katika taasisi hiyo.

ALAF Limited yazindua maonyesho ya kazi DIT
ALAF Limited, kampuni inayoongoza na inayoaminiwa kwa kuzalisha vifaa vya ujenzi Tanzania, Jumamosi ilizindua Maonyesho ya kazi kwenye Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DTI).

Meneja wa Rasilimali watu wa ALAF Bw. Jumbe Onjero alisema uzinduzi huo wenye dhamira ya ‘Kujenga Madaraja’ ulilenga kukuza vipaji vya vijana ili kupata mafanikio katika maisha yao.

Bw Onjero alisema: "Dhamira ya ‘Kujenga Madaraja’ inaonyesha moyo wetu wa dhati wa kuanzisha mahusiano imara na ya kudumu na wanafunzi wetu, wanaojiandaa kwa kazi na kwa mahitaji ya tasnia,” alisema.

Kulingana na Bw. Onjero alisema maonyesho ya taaluma ni fursa nzuri kwa watu binafsi kusikia masimulizi ya mafanikio ya ukuaji wa kazi, kuwa na mtandao wa mawasiliano na wanataaluma hao, na kujifunza zaidi kuhusu ujuzi unaohitajika ili watu waweze kufikia malengo ya kazi zao.

Alisema baada ya DIT, ALAF inaarajia kwenda katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu, kama vile vyuo vikuu na vyuo vingine na shule za sekondari nchi nzima.
“Tukio la Jumamosi lilikuwa na hotuba kutoka nyanja mbalimbali, warsha shirikishi, na mijadala ya paneli, kipindi cha ‘maswali na majibu’ kilichoratibiwa vyema, kikiruhusu kushirikishana uzoefu binafsi wa washiriki.”

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Taaluma wa DIT aliipongeza ALAF Limited kwa kuanzisha maonyesho ya taaluma, akisema ni njia nzuri ya kurudisha kwa jamii ukarimu.

"Hii itahakikisha wanafunzi wetu wanajiandaa vizuri kukabiliana na soko la ajira na wanajua matarajio ya jamii kwao watakaofika huko kwenye soko," alisema.

Alitoa wito kwa wanafunzi kutumia fursa ya maonyesho kwa sababu matukio kama haya ni ya nadra sana kwani pia inawapa wanafunzi fursa ya kifahamu ukweli kuhusu Soko la ajira.

Alisema kitendo cha kuwaleta wanafunzi waliopita DIT na sasa wameajiriwa na ALAF kimewatia moyo wanafunzi wanaotarajia kumaliza masomo Yao.

Mmoja wa wanafunzi hao wa zamani, Injinia Tumaini Minja, alisema Programu hii ya ALAF ilimfungulia fursa kwani aliajiriwa mwaka mmoja baada ya kufanya kama majaribio na baada ya miaka Saba sasa anasimamia kitengo cha mabati ya rangi.

"ALAF imeona umuhimu wa kuajiri vijana wa kitanzania Kwa maana hiyo wameweka nguvu kubwa katika career fair ili wapate watu sahihi," alisema.

Waziri wa Miundombinu na Teknolojia wa DIT, Kelvin Wilson ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa nne anayesomea uhandisi wa umeme, alisema zoezi hili ni la kuigwa kwani litahakikisha ALAF inapata mainjinia wa uhakika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...