Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi( SACP) Ralph Theobald Meela akipokea tuzo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi( SACP) Ralph Theobald Meela akizungumza  kwenye kelele hicho.


Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
MKUU wa jeshi la Polisi nchini IGP Inspekta Jenerali Camilius Wambura amesema Jeshihilo nchini tayari limesambaza Askari Polisi Kata 3945 ili kuhakikisha usalama wa Watu wenye Ulemavu wa ngozi Albino nchini.

Ameyasema hayo katika kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya kuongeza uelewa juu ya Ualbino IAAD duniani ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Maimoja Wilayani Kibaha Mkoani Pwani ambapo IGP Wambura amewakilishwa Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ASCP) Raphael Meella amesema Jeshi la Polisi  limejipanga kusimamia na kulinda watu hao wenye Ualbino nchini ambapo tayari Askari Polisi Kata 3945 na Wakaguzi, Makamishina wakusimamia Polisi Jamii ili kuhakikisha usalama wao.

Meela amewataka kuendelea kufanya majukumu yao kwani Jeshi la Polisi lipo nyuma yao kwa kutumia njia za kiusalama na za kiinteligensia kuhakikisha wapo salama.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Watu Wenye Ulemavu Deogratius Ndejembi akiwa amewakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amezitaka Halmashauri nchini kutenga bajeti ya fedha kwaajili ya kununua Mafuta Kinga dhidi ya mionzi ya jua kwa Watu Wenye Ualbino kwakuwa jukumu la Halmashauri za wilaya nchini ni kuhudumia wananchi.

Amesema hayo ni maagizo ya serikali kwa Halmashauri zote nchini zihakikishe zinatenga bajeti ya fedha kwa ajili ya kununua mafuta kinga dhidi ya mionzi ya jua kwa watu wenye ualbino.

“Halmashuari zote zihakikishe zinatenga bajeti na fedha zinapatikana na fedha hizo zinanunua mafuta yenye kutoa kinga dhidi ya mionzi ya jua maana mnaweza kusema mmeweka kwenye bajeti lakini changamoto ni kwamba bajeti hiyo fedha haipatikani au fedha zikipatikana hazifanyi kazi ya kununua mafuta hayo”

“Hivyo tunaagiza fedha hizo ziwekwe kwenye bajeti na zipatikane na mnunue mafuta hayo kama ambavyo mnafanya kwenye huduma zingine na mfahamu hili ni la muhimu zaidi kwani linahusiana na uhai wa maisha ya wanadamu wenzetu” amesema Ndejembi.

Aidha akizungumzia ushiriki wa chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani kwa kusema “watu wenye Ualbino mnahaki ya kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi hivyo muitumie vizuri nafasi hiyo katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani”

Hata hivyo amesema serikali inaelekeza Maafia Elimu Maalumu na Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mikoa na Halmashauri nchini kuhakikisha wanafanya utambuzi wa watu wenye ulemavu wakiwemo watu wenye Ualbino na kufanya usajili wa watu hao wenye Ualbino orodha yao iwekwe kwenye kumbukumbu watu wenye ulemavu katika Ofisi za Watendaji wa Mitaa na Vijiji.

Awali Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino (TASS) Godson Mollel ameiomba Serikali kuwawekea nazingira ya usalama watu wenye Ulemavu wa Ngozi Albino nchini katika kuelekea kipindi cha Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika baadaye mwaka huu na Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2025.

Mollel amesema kipindi hili kuelekea chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu mwakani kundi hilo lihakikishiwe Ulinzi na usalama wao kwani kipindi hicho huwa na Matukio pengine ya hatari kwa kundi hilo la walemavu.

Mkurugenzi kitengo Cha huduma Kwa Watu Wenye Ulemavu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana ajira na Watu Wenye Ulemavu Rasheed Maftah amesema wataendelea kushirikiana nao Katika jamii.

Maadhimisho hayo yanefanyika kitaifa Mkoani Pwani ambapo yamefanyila Kwa siku tatu ambapo 13 June ndio kilele.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...