KATIBU Mkuu wa Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali ameiagiza Tume ya Madini chini ya Katibu Mtendaji wake, Mhandisi Yahya Samamba kuongeza kasi ya kutatua migogoro ya wachimbaji wa madini nchini.
Mahimbali ametoa maelekezo hayo leo Juni 27, 2024 alipotembelea Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) yanayoendelea katika Viwanja vya Jakaya Convention Centre (JKCC) jijini Dodoma.
Amesema, Tume inafanya kazi nzuri ya kukusanya maduhuli, mapato yameongezeka na yanaonekana na kuitaka iongeze kasi ya kutatua changamoto za wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwa wanachangia asilimia 40 ya mapato katika Sekta ya Madini
" Msi -ignore wachimbaji wadogo, STAMICO hata kama ni walezi na nyie Tume mna 'role' yenu, " amesema Mahimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...