Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na askari wa idara ya uhamiaji ya nchini Burundi wakati wa ziara ya ukaguzi wa Mpaka wa Manyovu unaotenganisha nchi ya Tanzania na Burundi.Waziri Masauni yuko katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Nhayalina akimuonyesha eneo lililovamiwa na raia wa Burundi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kushoto) wakati wa ziara ya kukagua Mpaka wa Manyovu unaotenganisha nchi ya Tanzania na Burundi.Wengine ni ujumbe ulioongozana na Waziri Masauni katika ziara hiyo mkoani Kigoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Na Mwandishi Wetu,Manyovu
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni ametoa mwezi mmoja kwa Idara ya Uhamiaji nchini kuhakikisha Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Mipaka kufanya kazi katika Kituo cha Uhamiaji Manyovu ili kuepusha upotevu wa mapato ya nchi,kuepusha mifumo ya rushwa na kudhibiti uingiaji wa watu wanaoweza kuhatarisha amani ya nchi……

Ametoa kauli hiyo baada ya kukagua shughuli za uingiaji na utokaji wa raia na wageni wanaokwenda nchini Burundi kupitia Kituo cha Uhamiaji Manyovu kilichopo katika Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ambapo pia amewataka kuhakikisha wanadhibiti vipenyo mbalimbali vinavyopatikana katika mpaka huo.

‘Lengo la Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuviwezesha vyombo vya ulinzi na usalama na hilo ameshalitekeleza na mtaona jinsi alivyowapandisha vyeo askari wa ngazi mbalimbali lakini sasa wajibu uenda sambamba na haki kwahiyo lazima muongeze jitihada katika kufanya kazi zenu,haiwezekani Waziri ndio aje hapa kufuatilia suala la mfumo,mara sijui mfumo wa kiyoyozi aufanyi kazi,sasa nishamuelekeza Kamishna Jenerali kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja mfumo huo unafanya kazi,haiwezekani serikali imewekeza fedha nyingi katika mfumo huu wa uhamiaji mtandao sasa haiwezekani leo usiwe unafanya kazi mnakaa kubeba fedha za wananchi na kuzipeleka benki kwa njia ya kawaida’ alisema Waziri Masauni

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Kaimu Mfawidhi wa Kituo cha Manyovu,Inspekta Arnold Masha aliweka wazi hali ya uingiaji na utokaji wa wageni kupitia kituo hicho ambapo jumla ya wageni na raia wa Tanzania 38624 waliingia na kutoka nchini kupitia mpaka wa Manyovu na jumla ya wakimbizi rai awa Burundi 3667 walipita katika mpaka huo wakirejea nchini kwao kwa hiari tangu Machi mpaka Mei 2024 huku Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Kanali Michael Nhayalina akiahidi kuimarisha utendaji na kuyafanyia kazi maagizo ya serikali yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...