Rais wa Internet Society Tanzania (ISOC) Nazar Kilama akizungumza katika mafunzo ya vijana kuhusiana na usimamizi wa Mitandao iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Thadei Nkazabi wa Taasisi ya Digital Opportunity Trust (Dot) akitoa maada kuhusiana na matumizi ya usimamizi wa Mtandao kwa Vijana yaliyoandaliwa na ISOC Tanzania.
Baadhi ya washiriki vijana katika mafunzo ya usimamizi wa Mtandao yaliyoandaliwa na ISOC Tanzania jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
TAASISI ya internet Society Tanzania Chapter(ISOC-TZ) kupitia jukwaa la usimamizi wa mtandao Tanzania 'Internet Governance Forum(TzIGF)' imewataka vijana kujenga uwezo katika masuala ya usimamizi wa mitandao.
Hayo ameyasema Rais wa ISOC -Tz Nazar Kilama kuwa vijana ndio viongozi wa sasa hivyo wanahitaji kujengewa uwezo katika masuala ya usimamizi wa mitandao.
Amesema vijana wana nguvu ya kushawishi serikali kuweka usawa wa matumizi ya internet vijijini na mjini pamoja na kushauri gharama za vifurushi kushuka ili kila mtanzania aweze kupapta huduma za mawasiliano hayo.
"Vijana wakijengewa uwezo katika usimamizi wa mtandao pamoja na kusimamia mtandao ndio daraja la kufanya kuwepo usawa wa matumizi kutokana vijana kuwepo katika sehemu za maamuzi na kufanya kurahisisha michakato yake"amesema Kirama
Hata hivyo amesema kuwa katika upatikanaji wa huduma za mtandao katika baadhi ya maeneo hawapati kwa ubora ambapo jukumu la vijana hao wanawajibu kushauri watunga sera juu ya kupata uwiano.
Naye Janeth Kahindi kutoka Taasisi ya TECH and Media Convergency (TMC), amesema mafunzo ni muhimu kwani Dunia ipo katika ulimwengu wa kidigitali hivyo itasaidia vijana kufahamu haki za kimtandao, mipaka pamoja na sheria.
"Ni muhimu zaidi kwa vijana kujifunza masuala haya kwasababu wengi wao wanatumia internet katika mambo mbalimbali ikiwemo kutengeneza ajira na pia vijana ni kizazi cha kesho itasaidia kuwa na kizazi salama.
"Nitoe wito kwa wadau wengine kuendelea kutoa mafunzo kama haya lakini pia niwashauri vijana wenzangu kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza katika kujifunza kuhusu masuala mazima ya kimtandao kwani kwa sasa yana nafasi kubwa katika jamii," amesema Janeth.
Kwa upande wake, Cyidion Cylivanus kutoka Chuo cha Mipango, amewashukuru ISOC kwa mafunzo hayo, ambapo amesema matumizi ya intaneti yanakuwa kwa kasi hivyo yanapaswa kuwa na faida kwa vijana na sio anasa.
"Gharama ya intaneti zikiwa kubwa vijana hawataweza kuitumia katika kuwaingizia kipato badala yake matumizi hayo yatageuka kuwa anasa kufanya vijana kuwa nje"amesema Cylivanus.
Amesema kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya internet kwenye dunia ya teknolojia kwa vijana wanatakiwa kuchechemua katika maeneo ya utoaji wa elimu kuhusiana na matumizi sahihi ya mtandano yasiyoacha madhara baada ya kutumia
Ameongeza kuwa katika kutumia mitandao kwa vijana kuachana na kuchapisha kwa kushirikisha watu wengine kwani madhara yake ni makubwa kwa mtu mwenye faragha pamoja na jamii inayomzunguka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...