MKUU wa Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi Mhe. Mohamed Moyo amewataka wafanyabiashara kuacha tabia ya kupanga bei mbili moja ya risiti na nyingine ya bila risiti jambo ambalo ni kinyume cha sheria. 

Mhe. Moyo amesema hayo leo tarehe 14.02.2025 ofisini kwake alipotembelewa na timu ya maofisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliofika kujitambulisha kabla ya kuanza zoezi la kutoa elimu ya kodi mlango kwa mlango kwa wafanyabiashara wa Nachingwea mjini.

"Ninawasihi wafanyabiashara kuacha mara moja tabia ya kuuza bidhaa moja kwa bei mbili yaani anayedai risiti anauziwa kwa bei ya juu na asiyedai risiti anauziwa kwa bei ya chini, mtindo huu ni siyo mzuri na unashusha maendeleo ya nchi yetu."  

Mhe. Moyo ameongeza kuwa, maendeleo yanayoonekana katika jamii kama vile barabara, ujenzi wa shule na miundo mbinu mbalimbali ni matokeo ya kodi inayolipwa na wafanyabiashara pamoja na wananchi kwa ujumla  na amesisitiza kwamba, hakuna taifa linaloweza kuendelea na kujitegemea bila ya wanachi wake kulipa kodi.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...