Na Nihifadhi Abdulla, Zanzibar

ZANZIBAR itaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini tarehe 28 Aprili 2025, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) ya kukuza mazingira salama na yenye afya kwa wafanyakazi

Akitoa taarifa la Umma Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mhe. Shariff Ali Shariff, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua mchango wa teknolojia katika kuleta maendeleo, lakini pia changamoto zinazokuja nayo zinahitaji uelewa na mwelekeo wa kisera, ameisisitiza kuwa hakuna maendeleo ya kweli bila kulinda afya na maisha ya wafanyakazi.

Waziri sheriff amesema ni vyema jamii kutambua umuhimu wa kuwekeza katika mifumo ya kisasa ya usalama na afya kazini ili kukabiliana na matukio yasiyotarajiwa yanayoweza kuhatarisha maisha ya wafanyakazi “Hii ni fursa ya kipekee ya kutafakari, kujipanga, na kuwekeza katika mifumo imara ya usalama na afya kazini ili kuhimili matukio yasiyotaribika yanayoweza kuharibu maisha ya wafanyakazi wetu,” amesema.

Katika orodha ya teknolojia muhimu, Waziri alitaja matumizi ya otomatiki ya kazi, vifaa mahiri kama kofia za kielectroniki na mavazi yenye sensa, na mfumo wa ufuatiliaji wa moja kwa moja (real-time monitoring) kupitia Internet ya Vitu (IoT), ambayo alisema inaweza kugundua mabadiliko au hatari kazini mapema.

Ameongeza Kwa kusema kuwa “Tutumie teknolojia kama chombo cha kulinda maisha na afya za wafanyakazi wetu. Taifa lolote linajengwa na watu wake, na watu salama ni msingi wa maendeleo endelevu.”

Aidha ameeleza kuna hatua kadhaa Serikali ilizochukua, ikiwemo kuboresha sera na miongozo ya OSH, kutoa mafunzo kwa wakaguzi, kuhamasisha uwekezaji katika teknolojia salama, na kuhakikisha teknolojia hazibagui bali zinajumuisha watu wa makundi yote ya jamii.

Waziri Shariff ametoa wito kwa waajiri wa sekta binafsi kuwekeza kwenye afya ya wafanyakazi si tu kwa bima bali pia kwa afya ya akili, ushauri nasaha, na mazingira ya kazi yanayothamini utu wa binadamu huku akiwahimiza wananchi kutambua umuhimu wa kuwekeza katika mifumo ya kisasa ya usalama na afya kazini ili kukabiliana na matukio yasiyotarajiwa yanayoweza kuhatarisha maisha ya wafanyakazi "Toeni vifaa vya kinga, wekeni sera madhubuti za usalama na hakikisheni mazingira bora ya kazi," amehimiza

Haya hivyo amewataka wafanyakazi kufuata maelekezo ya usalama, kutumia vifaa vya kujikinga, na kutoa taarifa za hatari kazini mara moja, Huku akitaabahisha kuwa usalama ni jukumu la pamoja, si la Serikali peke yake.

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba, Sheria na Utawala Bora Dkt Haroun Ali Suleiman atakuwa Mgeni Asmi katika Maadhimisho hayo yatakayofanyika kijiji cha Kizimkazi Wilaya ya kusini Mkoa wa Kusini Unguja na yatahusisha washiriki kutoka sekta binafsi na Serikali Kauli mbiu kwa mwaka huu ni: “Teknolojia mpya na mustakabali kwa Usalama na Afya Kazini”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...